Katika hali isiyo ya kawaida, watu wa mji wa Kaharisi nchini Uturuki
wameshuhudia tukio la ajabu la kuzaliwa kitoto kichanga cha miezi saba
baada ya mama yake kunyongwa. Kwa mujibu wa habari zilizotolewa, mtoto
huyo wa kiume amezaliwa akiwa na afya nzuri. Habari zaidi zinasema kuwa,
daktari wa gereza aliukimbilia mwili wa Sabah Mosilibasa, mwenye umri
wa miaka 28 baada ya kujifungua mtoto huyo, huku akikata roho. Aidha
habari zinasema kuwa, hadi mwanamke huyo anatiwa kitanzi, hakuna
aliyekuwa anajua kwamba alikuwa na ujauzito wa miezi saba, kutokana na
unene wa mwili wake, suala ambalo limezidi kuwashangaza watu. Sabah
alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa sumu mumewe
na watoto wake wawili na alisalia gerezani kwa muda wa miezi mitatu
akisubiri hukumu dhidi yake. Duru za habari zinasema kuwa, watu
walishangaa baada ya kuwekwa kamba ya kitanzi shingoni mwake na
kufyatuliwa kitanzi, kama ishara ya kumalizika adhabu hiyo, lakini
Mosilibasa aliendelea kutikisika miguu licha ya kwamba adhabu hiyo
ilikuwa imemashatekelezwa dhidi yake. Muda mchache baadaye alizaa mtoto
wa kiume ambaye awali alidhaniwa kuwa naye ameshakufa, lakini baada ya
kumsaidia pumzi mtoto huyo aliweza kupumua na kisha kupiga ukelele
CHANZO:IRANI SWAHILI
CHANZO:IRANI SWAHILI
Blogger Comment
Facebook Comment