Marehemu Dk. Sengondo Mvungi enzi za uhai wake.
Marehemu Dk. Sengondo Mvungi alipokuwa ICU katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Habari za kusikitisha zilizotufikia jioni hii zinasema kuwa Dk.
Sengondo Mvungi amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark Afrika
Kusini alikokuwa akitibiwa. Dk. Mvungi alipelekwa wiki iliyopita Nov. 7
mwaka huu kwa ajili ya kupewa matibabu zaidi akitokea Hospitali ya
Muhimbili kitengo cha MOI ambako muda wote alikuwa hajitambui baada ya
kushambuliwa na majambazi na kuumizwa vibaya sehemu ya kichwani akiwa
nyumbani kwake Kibamba. Wakati Dk. Mvungi anafariki, jana Jeshi la
Polisi, kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi,
lilitangaza kuwakamata watuhumiwa 9 wakiwa na mapanga yaliyotumika
katika uvamizi huo.Mpaka mauti yanamfika, Dk. Mvungi alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na Mhadhiri Mwandamzi wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB).
Marehemu aliwahi kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMEEN!
CHANZO:global publishers
0 comments :
Post a Comment