PART ONE
JUMANNE iliyopita Kaimu
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are maarufu kama Mzee Kinesi mbele ya
waandishi wa habari alitangaza kamati ya utendaji ya klabu hiyo kukubaliana
kumsimamisha mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Rage alisimamishwa
baada ya kamati hiyo kutoridhishwa na utendaji wake lakini kuu ni kukataa
kipengele cha marekebisho ya katiba ya klabu hiyo. Mambo yametajwa kumuhusu
Rage lakini mengine ni juu ya uuzwaji wa wachezaji Emmanuel Okwi na Mbwana
Samatta na sambamba na mkataba wa Azam TV.
Mapinduzi hayo yasiyo
rasmi yalitangazwa wakati Rage akiwa Sudan katika vikao vya kamati za bunge za
Afrika zinazoshuhulika na hesabu za serikali hivyo wakati uamuzi huo
unatangazwa Rage hakuwepo nchini.
PART TWO
Ijumaa ya Novemba 21,
2013 Rage aliwasili nchini kutoka Sudan akiwa na donge moyoni mwake, na kwa
bahati nzuri aliwasili salama uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam huku akilakiwa na kundi la mashabiki wachache wa klabu yake.
Apanda ndege moja na
Hanspope
Rage aliwasili nchini
na ndege ya Shirika la KQ majira ya saa 1:30 akitokea Nairobi ambako
aliunganisha ndege akitokea Sudan na kwa bahati alipanda ndege moja na
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hanspope.
Hanspope alikuwa wa
kwanza kutoka uwanjani hapo na kudakwa na waandishi wa habari waliotaka kujua
sababu za yeye kuwepo uwanjani pale, na moja kwa moja alijibu kwamba; “Mimi
nimetoka Lubumbashi (DR Congo) katika biashara zangu na Rage nimepanda naye
ndege moja.”
Aliongeza; “Nimekaa
naye jirani kabisa na tumezungumza mengi lakini nimemuhakikishia kwamba nilikuwepo
kwenye kikao cha kamati kilichomsimamisha.Msubirini aje hapa mzungumze naye
tena msimsubiri hapo maana yeye anatokea VIP.”
Baadaye saa 1:45 Rage
alichomoza katika lango la VIP na moja kwa moja alikutana na kundi la mashabiki
wa Simba na waandishi wa habari ambao walimuhoji maswali lukuki lakini
alisimamia msimamo wa kuozungumza hadi kesho yake (jana jumamosi).
“Nashukuru nimefika
salama na napenda kuwaambia kwamba mimi ndiye mwenyekiti wa Simba hakuna mtu
mwingine mwenye cheo hicho,” alipoulizwa zaidi kuhusu uamuzi wake juu ya
maamuzi hayo ya kamati, Rage alisema; “Unajua rafiki yangu Zitto Kabwe amepata
matatizo ya kusimamishwa katika chama chake kwa hiyo sipo katika mood ya kujibu
maswali mengi.”
Rage akasema; “Kesho
Jumamosi nitazungumza na waandishi saa saba kamili.”
Aondoka na kamsafara zake
Baada ya kauli hiyo,
Rage aliondoka uwanjani hapo na gari aina ya Toyota Granvia lenye namba za
usajili T 300 CPR. Gari hilo lilifuatiwa na mabasi matatu yenye uwezo wa
kuchukua abiria wasiozidi 25 ambalo la kwanza lilikuwa na namba za T 885 BNT, T
208 BFM na lingine lenye namba T 549 BZQ.
Msafara huo wa Rage
ulienda hadi makao makuu ya klabu hiyo ambapo ulisimama kwa muda kisha
ukaondoka klabuni hapo huku kila mmoja akidhani kesho Rage atatoa neno.
PART THREE
Huku umma ukiwa na
shauku ya kufahamu kitakachozungumzwa na Rage, asubuhi ya Jumamosi ya jana,
likatoka tangazo kwamba, Rage hasingeweza kuzungumza siku hiyo na badala yake
atafanya hivyo leo Jumapili.
Sababu kubwa ya Rage
kutozungumza jana ilisemwa ni yeye kupata nafasi ya kwenda TFF kupeleka barua
yake ya kuelezea mchakato wake wa kusimamishwa ikiwa ni baada ya Mzee Kinesi
kupeleka barua ya kumsimamisha Rage.
PART FOUR
Mungu si Athuman, TFF
ikaona Rage ana hoja na moja kwa moja ikamuagiza aitishe mkutano wa wanachama
ndani ya siku 14 ili kumaliza tofauti za kiungozi zilizopo.
TFFilitoa agizo hilo
baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja
kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine
kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Uamuzi wa TFF ulifanywa
kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club
ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA,
na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”
TFF ikasema itatuma
wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba
kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.
PART FIVE
Leo hii Rage amesema
hawezi kuitisha mkutano mkuu wa dharura kama alivyoelekezwa na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kwa kuwa shirikisho hilo halina mamlaka ya kufanya hivyo.
Rage alisema TFF
haiwezi kumlazimisha kufanya hivyo na ikiendelea kumlazimisha kufanya hivyo
atajiuzulu nafasi yake kwani amechoka kuona anaonewa kila siku.
Kina Mzee Kinesi
walikaa kikao cha harusi
“Watu walionisimamisha
wanasema ni maamuzi ya kamati ya utendaji, hii siyo kweli kile hakikuwa kikao
cha kamati ya utendaji bali ni kikao cha kawaida tu kama kikao cha harusi.
“Katiba ya Simba ibara
ya 28 (1) kuanzia a, b, c mpaka d inasema wazi kwamba, maana ya kamati ya
utendaji ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe saba. Na kamawakitaka kukaa,
mwenyekiti ndiye mwenye jukumu la kuitisha kikao au makamu mwenyekiti kwa
ridhaa ya mwenyekiti kama akiona kuna ulazima wa kufanya hivyo,” alisema Rage.
Rage alisema katiba ya
Simba inamtaka mwenyekiti kuitisha vikao vinne kwa mwaka, yaani kimoja kila
baada ya miezi mitatu.”Sasa mimi nimeshaitisha vikao 12 ndani ya mwaka huu,”
alihoji Rage.
Aidindia TFF, aishangaa
kuwatambua kina Kinesi
Rage anasema alipeleka
barua yake TFF kuelezea uhuni huu uliofanywa na hao watu, lakini anashangaa kwa
nini TFF hawakutoa tamko lolote la kulaani kinachoitwa mapinduzi na badala yake
wanamlazimisha kuitisha mkutano.
“Katika katiba ya
Simba, Ibara ya 22 inaelezea kuhusu mkutano mkuu, haya si maneno yangu lakini
nanukuu hapa, inasema mwenye wajibu wa kufanya hivyo ni mwenyekiti kwa
kushirikiana na kamati ya utendaji kama anaona inafaa. Sasa hili la maelekezo
ya TFF linatoka wapi?,” alihoji Rage.
Adai kuna mbaya wake TFF,
wakimzingua anajiuzulu
Rage anasema kuna
kiongozi mmoja yupo ndani ya TFF ambaye zamani alikuwepo Simba na akashindwa
akaondoka zake lakini sasa ndiye anayemchafua ili tu aweze kurejea Simba lakini
yeye anamuachia mungu.
“Kuna kiongozi mmoja
aliyekuwa Simba na sasa yupo ndani ya kamati ya utendaji ya TFF, huyu ananiandama
na kunichafua kila siku. Niliwapelekea TFF barua ya mambo yote haya na ilipaswa
kamati ya maadili ipitie lakini badala yake kamati ya utendaji ndiyo iliyofanya
kazi hiyo, hakuna kitu kama hicho. Sasa wakiendelea kulazimisha mkutano mimi
nitajiuzulu.”
“Tazama mfano huu, wakati
uchaguzi wa TFF ulipoingia katika mgogoro kwa baadhi ya wagombea, Fifa ilielekeza
uchaguzi huo ufanyike baadaye lakini si kwa kuipangia TFF kama wanavyoniambia
mimi,” alisema Rage na kuongeza.
Amuingiza vitani Wambura,
ampa ulaji Malkia wa Nyuki
Rage kabla hajamaliza
mkutano wake na waandishi wa habari alitangaza kumteua Michael Wambura kuwa
mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba na huku akimtaja Rahma Al Kharoos kuwa
mjumbe wa baraza la wadhamini la Simba.
“Namtangaza Michael
Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, huyu anachukua nafasi ya malkia
wa nyuki (Al Kharoos) aliyeniomba kutolewa katika kamati hiyo kutokana na
kubanwa na kazi zake.
“Nimemuomba malkia wa
nyuki aingie katika baraza la wadhamini na kuanzia sasa yeye atakuwa mmoja wa
wajumbe wa baraza la udhamini na jina lake nitalipeleka likathibitishwe na
mkutano mkuu hapo baadaye,” alisema Rage.
Kwa uteuzi huo ina
maana Rage sasa atakuwa na mjumbe mmoja anayemuunga mkono ambaye ni Wambura.
Wambura huyu anaelezwa kutowakubali Friends of Simba kundi linaloiongoza Simba
kwa sasa.
Awaacha waandishi bila
kujibu maswali, aondoka nchini
Muda mfupi baada ya
mkutano huo na waandishi wa habari, Rage aligeuka mbogo kwa kukataa kujibu
maswali ya waandishi wa habari huku akisema anayetaka kuandika habari hiyo
naandike na asiyetaka aachane nayo.
“Sitaki maswali hapa, anayetaka
kuandika aende kuandika na asiyetaka aache, wengi humu mnatumiwa na hawa watu,
sasa ni kipi mtakachoniuliza?, sitaki swali tuondoke,” alisema Rage huku
akinyanyuka.
PART SIX
Mtandao huu
uliwasiliana na TFF ambapo kaimu katibu mkuu wake ndiye aliyepatikana na
aliposomewa maamuzi ya Rage, akasema hakuna tatizo kwa Kamati ya Utendaji ya
TFF kutoa uamuzi huo hivyo si kweli kwamba hawakuwa sahihi kutoa maelekezo hayo
kwa Rage.
Wambura alisisitiza
kwamba, wanasubiri siku 14 ziishe halafu wachukue uamuzi endapo mkutano mkuu
hautafanyika ndani ya Simba.
“Sisi tunangoja siku 14
zipite halafu utaona tunafanya kitu gani leo ndiyo kwanza siku ya pili, yeye kama amesema
hivyo wacha tungoje siku 14 ziishe halafu tutakuwa na uamuzi wetu,” alisema
Wambura.
USIKOSE PART SEVEN
BAADA YA SIKU 12 zijazo
Blogger Comment
Facebook Comment