-->

MCHEZAJI WA TIMU YA WANAWAKE WA KOREA ATILIWA SHAKA KUWA NI MWANAUME



Mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Korea  Park Eun-Seon anashtumiwa ya kwamba huenda kawa ni mwanaume.Hali hii imejitokeza sasa na imekuwa ni jambo la kushangaza kwani mchezaji huyo amekuwa akichezea timu ya wanawake ya Seoul City Hall kwa muda mrefu pia aliichezea timu ya taifa ya Korea mwaka 2003 na 2004 katika olympics.Seoul City Hall imekuwa na mafanikio mazuri kwani imeshika nafasi ya pili na  Park Eun-Seon ameshinda mabao 19.
Hakuna kipimo chochote kilichotumika kutambua jinsia ya Park mpaka sasa ingawa bado kuna mzozo wa chini kwa chini kwa timu mbali mbali huku ikihisiwa huenda kukawa na mgomo wa wachezaji kuhitaji kuthibitishiwa jinsia halisi ya Park kwa kuhofia kuumizwa kutokana na kuonekana kuwa ni imara na mkomavu kama mwanaume.
chanzo:I Am KoreAm
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment