-->

HII NDIO HABARI YA FARAJA KUTOKA TANESCO,SOMA MWENYEWE

WAKATI watanzania akiendelea kuteswa na mgao wa umeme, uliotokana na matengenezo katika mitambo ya kusafisha gasi kupeleka katika mitambo ya Shirika la Kusambaza Umeme Tanzania,(Tanesco),Mkurugenzi wa Shirika hilo Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kwamba, ukali wa mgao huo utaanza kupungua leo usiku baada ya mafundi wanaoshugulikia mitambo hiyo kukamilisha kazi yao kwa asilimia 80 ndani ya simu tano kati ya 10 zilizotangazwa awali.
 Mkurugenzi wa Tanesco Mhandisi,Felchasmi Mramba akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Badra Masoud picha na Habarimpya.com
Akizungumza na Habarimpya.com jijini Dar es Salaam,Mhandisi Mramba alisema kwamba, awali walitegemea kwamba kazi hiyo itakamilika ndani ya siku 10 zilizotangazwa awali, lakini kutokana mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani siku tano za mgao huo, wameamua kupunguza muda wa mgao na kwamba hali hiyo itaanza kuonekana leo.
"Awali tulitarajia kwamba kazi hiyo ingekamilika ndani ya siku 10, kama tulivyo tangazwa awali lakini kutokana jitihada za mafundi wanaoshugulikia suala hilo kuzaa matunda ndani ya siku tano, tumeamua kuwatangazia wananchi kwamba makali ya mgao huo utanza kupungua nguvu leo jioni"alisema Mhandisi Mramba.
CHANCHO:HABARI MPYA
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment