Siku
moja baada ya chama cha Demokrasia na maendeleo- Chadema kuwavua
nyadhifa zote za uongozi aliyekuwa naibu katibu mkuu wake Mh. Zitto
Kabwe na wenzie wawili kufuatia tuhuma za kukihujumu chama hicho Mh.
Zitto amesema ataendelea kuwa mwanachama mtiifu na atayaheshimu maamuzi
yaliyotolewa ili kukiimarisha chama hicho.
Mh. Zitto Kabwe aliyeongozana na mwenzie Dr.
Kitilla Mkumbo amesema hayupo tayari kuona chama chake kinapoteza
mwelekeo kwani ndio chama pekee kilichomkomaza kisiasa na kuahidi
kutumia njia mbadala ya kidemokrasis kuhakikisha tofati yake na chama
hicho itakwisha ili kukiimarisha chama hasa kipindi hiki cha kuelekea
kwenye uchaguzi na kuonya mipasuko ndani ya chama yaweza ongeza
mafanikio kwa chama kingine ambapo amewahakikishia Watanzania na
wanachama wake kuwa hayo yataisha na Chadema itaendelea kutetea haki za
wanachi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu Dr.
Kitilla Mkumbo amekiri kuandaa waraka huo akishirikiana na mwenyekiti
Chadema mkoa wa Arusha Samsoni Mwigamba uliolenga kubadilisha uongozi
wa juu wa chama hicho kidemokrasia na kukiri kutaka kujiuzulu bila
mafanikio na kuongeza kuwa Mh. Zitto aliyetambulika ndani ya waraka huo
kama “mm” yani mhusika mkuu hakuwa anajua chochote kuhusiana na waraka
huo hata hvyo Dr. Kitilla amekataa kumtaja mhusika mwingine aliyetajwa
kama m2 ambapo m1 alikuwa yeye na m3 akiwa Samasoni.
Nao baadhi ya wafuasi wa chama hicho wameelezea
kufurahishwa na hatua wakiyoichukuwa viongozi wao na kuwa ni kitendo cha
uzalendo na kukomaa kisiasa na kutoa wito kwa chama hicho kuepuka
migongano ili kukikuza kwa maslahi ya taifa.
Blogger Comment
Facebook Comment