Marekani imeyaorodhesha rasmi makundi ya wanamgambo ya Nigeria ya Boko Haram na Answar katika orodha ya makundi ya kigaidi.
White House pia imetoa amri ya kuzuiwa fedha na mali za makundi hayo mawili, yanayotuhumiwa kusababisha vifo vya maelefu ya watu kaskazini na katikati mwa Nigeria.
Marekani imedai kuwa imechukua hatua hiyo kwa kuwa inatiwa wasiwasi na kukosekana usalama nchini Nigeria na kwamba machafuko yanazorotesha uwekezaji nchini humo na pia kusambaa hadi kwenye nchi jirani.
Jeshi la Nigeria limekaribisha hatua hiyo ya Marekani ambapo Brigedia Christ Olukolade msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa, uamuzi huo unatia moyo na kwamba ni hatua nzuri inayoleta maelewamo katika kuimarisha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.
Kundi la Boko Haram pamoja na la Answar lililojitenga kutoka kundi hilo kwa muda mrefu yamekuwa yakihesabiwa kuwa tishio kubwa kwa usalama wa Nigeria.

CHANZO:AHBAABUR
0 comments :
Post a Comment