-->

JUMUIA YA UAMSHO YAIKANA FACEBOOK PAGE INAYOTUMIA JINA LAO

"Sisi kama Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) hatuna kabisa mtandao wa facebook ule mtandao wenye jina letu sio wetu sisi na wala hatuna mahusianao nao ni watu tu wenyewe wameamua kuanzisha lakini hakuna kiongozi hata mmoja wa UAMSHO ambaye anautambua wala kuukubali kwa maana hiyo hatuhusiki kabisa na mtandao huo na ndio maana kinachoandikwa humo hatukijui wala hatukubaliani nayo maneno ambayo yanachochea ubaguzi, uhalifu na yasiozingatia hekima na busara na na ni kinyume na maagizo ya dini yetu ya Kiislamu" Sheikh Azzan Khalid Hamdan Amiri wa wa Jumuiya hiyo amesema akiwa nyumbani kwake Mfenesini Unguja.(kipande hiki kimenukuliwa kutoka Islamic Forum in facebook)
Hii ndio moja ya post iliyoandikwa na watu wanaojiita
Jumuiya Ya Uamsho na Mihadhara Ya Kiislamu Zanzibar 
kwenye facebook
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment