Baada ya kuzagaa taarifa za kuwa mtoto wa Gaddafi, Saif
al Gaddafi ametoroka katika jela aliokuwa amewekwa, kituo cha
televisheni cha Al assema cha nchini Libya kimeonesha video ya mahojiano
na Saif wiki iliyopita.
Hii ni mara ya kwanza Saif al Gaddafi kuonekana katika televisheni ya Al-assema ya Libya tangu kukamatwa kwake mwaka 2011.
Mahojiano
hayo yalifanyika ndani ya jela aliofungwa huko kusini mahgaribi mwa mji
mkuu wa nchi ya Libya. Kituo hiko cha televisheni kiliruhusiwa
kumuuliza maswali matatu tu.
Moja
ya swali aliloulizwa ni kuwa je anataka kesi yake isikilizwe Tripoli
badala ya Zintal ambapo ni kilomita 180 toka mji mkuu. Alijibu kwamba
Zintah ipo ndani ya nchi ya Libya kwa hiyo hakuna tofauti na Tripoli.
Waasi wa Zintah ndio wanaomshikilia Saif al Gaddafi na wamekataa kumpeleka katika mahakama ya mji wa Tripoli. Muda wote aliokuwa akiongea Saif al Gaddafi alikuwa akiweka mkono wake juu ya mdomo kuficha sehemu iliyong'oka jino lake la mbele.
Mtoto
huyo wa Marehemu Gaddafi, alionekana ni mwenye afya njema akiwa amekaa
katika kitanda na mavazi ya sare za jela ya rangi ya bluu. Hakuonekana
kuwa na raha muda wote wa mahojiano.
Wakati huo huo, Serikali
ya Libya imeombwa imkabidhi Saif al Gaddafi kwa mahakama ya kimataifa
ya uhalifu, ICC, ili afunguliwe mashtaka. Wito huo umetolewa na
Mwendesha Mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, wakati akilihutubia Baraza la
Usalama kuhusu hali nchiniLibya.
Bi
Bensouda amesema Libya imepiga hatua kadhaa kisheria, ikiwemo kuridhia
mkataba wa Rome, ambao uliiunda mahakama ya ICC. Hata hivyo, amesema
kesi dhidi ya Saif al Gaddafi bado inatakiwa kusikilizwa na mahakama ya
ICC, na kuiomba serikali yaLibya imkabidhi kwa mahakama hiyo.
“Jukumu
la kuwasalimisha kwenye mahakama watu ambao waranta za kukamatwa
zimetolewa dhidi yao ni lazima liheshimiwe. Hisia za kisiasa hazina
nafasi katika sheria, ikitumiwa kwa haki na uhuru. Natoa wito kwa
serikali ya Libya kumsalimisha Saif al Gaddafi kwa mahakama ya ICC bila
kuchelewa",alisema Bi Bensouda.
Bi
Bensouda ametoa wito kwa Baraza la Usalama liikumbushe na kuisihi
serikali ya Libya kuitikia maombi ya mahakama ya ICC, na kutoa wito kwa
nchi zote wanachama ziheshimu na kutekeleza maamuzi ya majaji wa
mahakama hiyo.
0 comments :
Post a Comment