Mwanamke
mmoja mkazi wa manispaa ya Shinyanga amejifungua mtoto wa ajabu wa kike
asiyekuwa na mdomo wala pua huku masikio yake yakiwa shingoni katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema
mtoto huyo alizaliwa jana saa moja asubuhi na alifariki muda mfupi
baadaye kutokana na kasoro alizokuwa nazo.
Mwandishi
wa habari Nunu Abdul amefuatilia kwa ukaribu zaidi habari
hii,Tutawaletea habari kamili hivi punde,ikiwemo sababu za kuzaliwa kwa
watoto wa namna hiyo.
Credit: Malunde1 Blog
0 comments :
Post a Comment