NA KAROLI VINSENT
JESHI la
Polsi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lipo katika hatua ya mwisho katika
kukamilisha ushahidi ili kumfikikisha mahakamani Katibu mkuu wa Chama
cha Demokrasia na maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa pamoja na
makada wa Chama hicho.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi
Kanda maalum Dar es Salaam Suleimani Kova ametaja sababu ya kumfikisha
mahakani katibu huyo wa Chadema na Makada wake inatokana na Vitendo
vinavyodaiwa ni vya kinyama alivyofanyiwa mlinzi wake vya
kumteka,kumpiga na kumlazimisha kutaja watu wanaomtuma kumuua Katibu
mkuu wa Chadema.Hivyo hivyo Jeshi hilo la Polisi limesema kwa sasa
linawashikilia makada watatu wa Chama hicho kikuu cha upinzani nchini
ambao ni Boniface Jacob miaka 32 mkazi wa ubungo kisiwani ambae pia ni
diwani wa kata ya Ubungo kupitia chama hicho.
Sambamba na Hemed Ally Sabula miaka 48 mkazi wa Tandale kwa tumbo ambaye anadaiwa ni Afisa Usalama wa chama hicho Taifa.
Mbali na
hao pia Kamishna Kova amemtaja Kada mwengine anayeshikiliwa kuwa ni
Benson Mramba,miaka 30,mkazi Tabata Kisukulu ambaye ni Afisa Utawala wa
Chadema.
Kamishna
kova amebainisha kuwa Ushahidi wao utakapokamilika mafaili yao
yatafikishwa kwa Wakili wa Serikali ili hatua zichukuliwe.
Aidha,Akizungumzia
sakata la Mlinzi Kagenzi amesema kwa sasa wanamalizia kazi ya kukusanya
ushahidi kutoka Chadema ambao wanamtuhumu bwana Kagenzi ambaye anafanya
ushirikiano na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM bara Philip
Mangula na Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni kwa kuaandaa mpango
wa kutaka kumuwekea sumu Dokta Slaa.
Kesi hiyo
kwa mala ya kwanza ilifika polisi tarehe 8 mwezi huu majira ya saa
11.jioni katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kupitia kwa wakili wa
Chadema anayetambulika kwa jina la john Malya akiambana na mtuhumiwa
Khalid Kagenzi ambaye ni mkazi wa Tandale kwa tumbo ambapo Wakili huyo
aliiambia polisi kwamba alimleta mtuhumiwa baada ya kuagizwa na Dokta
Slaa ili kutoa malalamiko kwa niaba yake.
Ambapo
Katika maelezo yake anadai Wakili huyo kuwa uongozi wa Chadema ulikuwa
ulichukuwa hatua mbalimbali dhidi ya kugenzi ikiwemo kumbana na
kujilidhisha kuwa nahusika na mipango ya kimauaji.
Kwa
mujibu wa Kamishna kova anasema katika mahojiano wakabaini kunavitendo
vya kinyama ambavyo mlinzi huyo wa Dokta Slaa amefanyiwa na Makada wa
Chadema baada ya Jeshi hilo kumkuta akiwa na majeraha mbalimbali katika
mwili wake
SOURCE
MATUKIO NA VIJANA
MATUKIO NA VIJANA
0 comments :
Post a Comment