-->

WASOMI WA VYUO VIKUU WAMUOMBA PRO:MUHONGO AGOMBEE URAISI

unnamed
Umoja wa Vyama vya wanafunzi elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali kanda ya kaskazini Kilimanjaro na Arusha wajitokeza kumshawishi Prof. Sospeter Muhongo kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mwaka 2015.(Picha na Jamiiblog).
unnamed (1)
Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake Mwenyekiti wa vijana  Charles Ngereza kutoka chuo cha Uhasibu Arusha amesema kuwa kinachowafanya kumshawishi Prof Sospeter Muhongo kugombea urais ni kutokana na kuwa kiongozi bora kwa wananchi na mtu anayejali matatizo ya wananchi katika kuwapatia huduma.
unnamed (2)
Pia wanasema kuwa amekuwa akiwezesha  uchumi kujitegemea na kupinga ulanguzi katika sekta ya uwekezaji pamoja na kutetea vijana katika uwekezaji na kupata ajira.
unnamed (3)
Vijana hao ambao ni umoja wa vyama vya wanafunzi wa elimu ya juu katika picha kutoka kushoto ni Nelson Wilson Machumu ,Tumaini University. 2 Daud Hipolity Shayo Chuo cha Uhasibu (Iaa)3 Sarah Aminirabi Mushi Arusha University 4. Charles Ngereza Chuo Cha Uhasibu Arusha.5. Hobeshi Juvenary Makumira University Pamoja na Rahma Yusuph Sengeza Chuo cha Jomo Kenyata.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment