TAARIFA KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU 2015/2016
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI,
SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU MWAKA 2015/16
JIHADHARI NA MATAPELI
Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu wapya kwa
mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015) linalodaiwa kuwa limetolewa
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao
ya Kijamii. Taarifa zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na
Wizara haihusiki nazo.
Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda kuufahamisha umma
kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti, Stashahada, na Shahada hufanywa
na Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira
kutoka Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.
Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa sahihi
kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha zitatangazwa na
Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI mara
watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
23 Machi, 2015
0 comments :
Post a Comment