Waziri wa
Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango wa
upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika Hospitali
Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO
Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati) Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Daktari
Asma Ame Hassan akimpima usikivu mtoto Nour Sabri Al hilal katika
uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga hafla iliyofanyika
Hospitali kuu ya Mnazimmoja.
Wafanyakazi
wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga
wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
Waziri wa
Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa
kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Baadhi ya
wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga
wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja.
Waziri wa
Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman amesema sikio, mdomo na macho ni
sehemu muhimu sana katika maisha ya binaadamu hivyo unapokuwa na
wataalamu wa kushughulikia viungo hivyo ni neema kubwa inayopaswa
kuenziwa.
Haya
ameyasema jana katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar wakati
wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga mara baadaya kuzaliwa
ili kujua matatizo yao.
Amesema
uchunguzi wa watoto wachanga kujua usikivu wao mapema ni mpango mzuri
ambao utalisaidia Taifa kuwa na watoto wenye usikivu mzuri na njia
rahisi ya kuwapatia matibabu kwa watakaogundulika na matatizo hayo.
"Kujua
tatizo la kiafya mapema na kuanza kulishughulikia kunapunguza gharama za
matibabu hivyo nawanasihi wazazi kuwapeleka watoto wenu mara baada ya
kujifungua, "alisisitiza Waziri wa Afya.
Amesema
maradhi ya usikivu yamekuwa yakiwasumbua watoto wengi Zanzibar na iwapo
kila mzazi atatimiza wajibu wake wa kumpeleka mtoto wake kupata vipimo
yataweza kupungua.
Waziri wa
Afya aliwataka wazazi kuwa na utamaduni wa kuzalia Hospitali ili kupata
huduma hiyo kwa urahisi na watakaozalia majumbani kuwapeleka watoto wao
kuchunguzwa usikivu mara baada ya kuzaa.
Aidha
Waziri huyo aliwataka madaktari waliopatiwa mafunzo ya kutoa huduma hiyo
kuwa waadilifu katika kutekeleza kazi zao kwani huduma za watoto
wachanga na wazazi zinahitaji uvumilivu.
Waziri
alisema tatizo la uskivu huazia mtoto anapochelewa kulia mara baada ya
kuzaliwa ama wanapopata homa ya manjano, kutopatiwa chanjo, mzazi
kuchelewa kuzaa baada ya uchungu wa muda mrefu na kuzaliwa mtoto bila ya
ya kufika muda wa kuzaliwa.
Nao
madaktari walio patiwa mafuzo hayo walisema kuwa wana uwezo mzuri wa
kuwapima usikivu watoto na kubaini matatizo yao na kuishauri Serikali
kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia watoto watakaozaliwa vijijini.
Mradi huo
wa kupima watoto usikivu ulipokea msada wa vifaa vya kisasa vya
uchunguzi kutoka Jumuiya ya Madaktari wanotoa huduma za matibabu
vijijini ( ZOP) ambavyo vina thamani vya Dola elfu 50 za kimarekani.
0 comments :
Post a Comment