IDADI ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi lililotokea jana nchini Tunisia imeongezeka na kufikia 23.
Mwananmke mmoja raia wa Uingereza ameongezeka na kufanya idadi ya watalii waliouawa kwenye shambulio hilo kuwa 18.
Mwananmke huyo ametambulishwa kwa jina la Sally Jane Adey wakati wa
mkutano na wanahabari uliofanywa leo na Wizara ya Afya nchini Tunisia.
Watu hao 23 wakiwemo watalii 18, raia wa Tunisia wawili na wapiganaji
wawili walifariki baada ya wapiganaji hao kuvamia jengo moja la
kumbukumbu za kihistoria liitwalo Bardo ambalo liko jirani na bunge
nchini Tunisia.
(Picha kwa hisani ya Daily Mail)
0 comments :
Post a Comment