Na Mwandishi wetu Mwanza
Mbwana Samata mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea TP Mazembe ya Congo ameisaidia Timu ya Taifa ya Tanzania isiaibike Nyumbani baada ya kusawazisha bao katika mechi ya kimataifa ya Soka kati ya Taifa Stars na Malawi.
Pambano hilo lililopigwa katika jiji la Mwanza uwanja wa CCM Kirumba lilimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku Stars wakitawala kwa kipindi kirefu bila ya mafanikio.
Goli la Malawi likifungwa dakika ya 4 na Esau Kanyenda mchezaji anayekipiga katika klabu ya Plolokwane City ya Afrika Kusini baada ya kipa wa Stars Mwadini Ali kushindwa kuudaka mpira wa kona huku Mabeki wakishindwa pia kumzuia mfungaji kupiga mpira ulioandika bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na kocha wa Taifa Stars Mrisho Ngasa aliyeingia kuchukua nafasi ya Haruna Chanongo na Salum Abubakari kuchukua nafasi ya Kiemba yaliisaidia Taifa Stars kupata goli la kusawazisha dakika ya 76 kupitia kwa Mbwana Samata akiitumia vizuri pasi Ya Mrisho Ngasa.
Licha ya kupiga mashuti 10 ambayo matano yalilenga goli Stars hawakufanikiwa kuongeza bao na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

0 comments :
Post a Comment