JESHI la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha kuhusika kwa Idara Usalama wa Taifa katika mipango ya kutaka kumuua Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dokta Wilbroad Slaa.
Kauli ya jeshi la polisi kanda hiyo ni kama inamjibu Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA (CC), Mabere Marando ambaye katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari alimtuhumu Naibu mkuu wa idara ya Usalama mkoa wa Kinondoni Elisifa Ngowi kuandaa mipango miovu kwa dokta Slaa akishirikiana na Mlinzi wa Katibu huyo bwana Khalid Kagenzi pamoja na Makumu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara,Philip Mangula.
Akikanusha taarifa hizo leo Jijini Dar es Salaam,Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati na mkutano na vyombo vya Habari amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi wakina ikiwemo kuchukua taarifa upande wa chama cha Chadema na Mlinzi wa Dokta Slaa na kubaini hakuna ukweli idara ya Usalama wa Taifa kuhusika.
“Tumefanya uchunguzi wa kina ikiwemo kuwahoji watu wote wanaotuhumiwa .Tumebaini kwa dhati kabisa hakuna mtu yeyote wa usalama wa Taifa aliyehusika katika mipango ya kumdhuru Dokta Slaa", Amesema Kamishna Kova.
Kamishna Kova ameongeza kuwa kwa sasa bado wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo na uchunguzi ukikamilika watafawakisha wahusika wote mahakamani bila kumwogopa mtu yeyote.
0 comments :
Post a Comment