-->

WANA CCM WAISHIO NJE YA NCHI WALALAMIKIA MABADILIKO YA UBINAFSISHAJI WA KAMPUNI YA UKAGUZI WA MAGARI

  • Viwango vya Kukidhi uhalali wa gari kuwa barabarani nchini Uingereza ni vya hali ya juu na havikwepeki kisheria.
  • Ni Jambo la kujifunza nyumbani na kuliwekea uratibu wa kisheria kwa kila baada ya muda fulani gari lazima liwe linafanyiwa Road Worthiness test na siyo kuliwekea kampuni binafsi hapa UK kwenye utaratibu unaofanya kazi.
 
Kituo cha kuthibitisha gari lako linakidhi ubora na usalama wa hali juu kuruhusiwa kutumika nchini Uingereza. MOT TEST CENTRE.
Mwanzo wa yote nataraji kuwa wote mko salama na mnaendelea vyema na uchapaji kazi kama kawaida.
Rejea kichwa cha habari hapo juu,tunaomba mtu peperushie hii habari ili wahusika wajue kitu wanachokifanya sio sawa na wasijaribu kutuburuza bila kutumia busara na kufuata sheria.
Ukitazama kwenye kiambatanisho cha habari hii utaona tangazo la TBS ambalo wanatangaza kuanzia tarehe 16/03/2015, Kuna kampuni binafsi inayomilikiwa na watanzania hapa nchini UINGEREZA (UK),ambao wanasemekana wameshinda zabuni ya kukagua magari yote yanayotarajiwa kuja Tanzania kwa gharama ya $200 kwa kila gari, hii ni uonevu na unyanyasaji kwa Watanzania wenzao, kwa sheria za hapa Uingereza (UK) kila gari linahitaji kukaguliwa na kutambulika kama linakidhi ubora wa kuendelea kuwa barabarani yaani (MOT) ambayo kwa sasa iko digital, kupitia link za DVLA au VOSA gonga hapa https://www.gov.uk/check-mot-status . Hii MOT inafanywa na wataalamu walio bobea, wenye sifa na vifaa maalum, kwa magari madogo vituo viko kila mji na kwa maroli na mabasi kuna vituo maalumu, kwa magari madogo gharama yake ni £50 tu .
Ukaguzi wa gari hufanyika kwa umakini na vifaa vya kisasa yaani “electronic diagnosis” kupima uchakavu kama kutu, emissions, na ubora wa kila kifaa muhimu katika gari.
Ukaguzi wa gari hufanyika kwa umakini na vifaa vya kisasa yaani “electronic diagnosis” kupima uchakavu kama kutu, emissions, na ubora wa kila kifaa muhimu katika gari.
Tunasikitishwa kwa kitendo cha TBS kutangaza mzabuni
huyu bila kufuata ushauri wa watanzania na wa kisheria ili zoezi zima liweze kukubalika na bila kuwaumiza watanzania. Iweje leo tulipie $200 kwa kampuni binafsi wakati kuna MOT yenye kiwango cha hali ya juu na kinachakubalika kwa standard za uhakika hapa UINGEREZA na kwingineko kuliko hii ya mtu binafsi isiyotambulika hapa Uingereza na kwa pesa kubwa zaidi?
 
Kwa kigezo kuwa kuna fake MOT hili ni jambo la kushangaza na la kupotosha sana kwani vituo hivi vinaendeshwa kielectroniki kwa log in appointement ya gari husika lanalohitaji kufanyiwa MOT na moja ya requirement ni kituo kuwa na CCTV ambayo ni connected on the system , hiyo link juu ni sehemu ambayo kila mtu anaweza tizama uhalali wa MOT kwa kila gari iliyotoka UK.
Kifungu kipi cha sheria kinatumika kuweka kiwango hiki?, kulikuwa na kesi imefikia wapi hadi leo watujulishe kuwa kuna mzabuni na gharama hizi kubwa. Hii ni aina ya uongozi usio jali maslahi ya watanzania na wasio weza wapunguzia mzigo wenzao kisa matakwa yao binafsi ya kujitajirisha tu. Mfano mzuri ni kuwa mtu yuko North katika miji kama Leeds au Sheffield, New castle, Manchester nk , ambako kuna vituo vya MOT lakini kwa utaratibu huu anapaswa kuleta gari yake London,Tulibury port kwenye ofisi hizi binafsi kisha atume gari yake.Wakati kuna vituo vya MOT kila mahali na kuna bandari North sio lazima kuleta gari London. Huu si uhungwana hata kidogo Zaidi ya kutizama maslahi binafsi.
Watanzania wote walioko UK wanapinga utaratibu huu mpya wa kuhujumu watanzania na kuomba serikali na shirika lake la viwango TBS kusitisha zoezi hili mara moja na kutizama utaratibu mzuri wa kutumia MOT yenye kiwango kinachokubalika na serikali ya hapa nchini UINGEREZA.
Uchunguzi wa gari ukiendelea ili kuthibitisha gari linakidhi viwango vya MOT hapa UK.
MOT ni ya kiwango cha juu sana na ndiyo maana uingereza hakuna ajali kama nyumbani ni jambo la kujifunza na siyo kuweka kampuni ya viwango hewa na kuongeza ajali nchini.
Kwa pamoja Watanzania wa UK wameanza kuweka sahihi ya kuomba kusitishwa utaratibu huu gonga hapa https://www.change.org/p/tanzania-goverment-foregn-affiars-tanzania-bureau-of-standard-tbs-to-stop-to-use-serengeti-freight-in-uk-for-vehicle-inspection-before-shipping-to-tanzania kwenda kwenye petition.
Tunaomba kuwajulisha wahusika hali hii haitaweza kukubalika kwa sasa wala baadae kwa kuwa huu ni mradi wa kunufahisisha watu wachache tu.Tunatanguliza shukrani kwa wana habari wote wenye kusambaza habari hii na kuomba wananchi wajiandikishe kupinga hali hii ya uonevu na unyanyasaji.
   Electronic and computerized diagnosis ya kila eneo la gari hadi matairi yana viwango vya kutumika.
Ni SISI wana Diaspora UKTZ.
NB; Link ya petition. Ikiwa hapo juu haipatikani
http://www.change.org/p/tanzania-goverment-foregn-affiars-tanzania-bureau-of-standard-tbs-to-stop-to-use-serengeti-freight-in-uk-for-vehicle-inspection-before-shipping-to-tanzania
 
 

Posted by; Abraham Sangiwa – Idara ya Itikadi na Uenezi – Chama Cha Mapinduzi – UINGEREZA.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment