Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT.
...Kumwaga ‘mboga’ mbele ya wandishi wa Habari Jumapili hii Machi 22
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Hayawi
hayawi…Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya
kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa
Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama
hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Hii
inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika
barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi
kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza
kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari Jumapili ya Machi 22.
tukio hilo litafanyika katika ukumbi wa Serena Hotel saa tano kamili asubuhi
ACT-Tanzania:
kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence
(ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar
es Salaam, Tanzania.
Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
Mwanachama rasmi wa ACT Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.
“He..he
he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi
hiyo kwa baadhi ya wanachama waliosimama (hawapo pichani) nje ya ofisi
za chama cha ACT tawi la Tegeta,
Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya kupokea kadi hito.
Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.
Mh. Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama hicho mapema leo.
Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa leo.
0 comments :
Post a Comment