-->

NAMNA YA KUTAJIRIKA KUPITIA UFUGAJI WA KUKU

BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU
Biashara ya ufugaji wa kuku ni biashara nzuri sana pia ni biashara yenye faida kubwa iwapo utawafuga vizuri na kuwahudumia ipasavyo. Mtaji wake ni mdogo unaweza kuanza na mtaji wa Tsh. 500,000 unatosha sana kuanzisha biashara hii.
Ili kuifanya biashara hii unahitajika kua na eneo la ekari 1 ukaweka mabanda ambayo yanaweza kuhifadhi idadi ya kuku wapatao 10,000
MAHESABU YA MAPATO NDANI YA MIAKA MIWILI
Anza kwa mtaji wa Tsh. 500,000 nunua kuku 25 ( kuku 20 yawe majike na jogoo 5) ambao utawanunua kwa Tsh. 250,000.00 wote 25. Hao kuku 20 watakapo anza kutaga kila kuku mmoja atatotoa vifaranga 10 kwa kila kuku mmoja, jumla kuku wote wataangua vifaranga 200. Ssa tuchukulie mfano katika vifaranga hivyo majike yanaweza kuwa 150 ambao ndani ya miezi 6 au zaidi nao wataanza kutaga. Kipindi hicho utakuwa na kuku 200 ambao walio totolewa na wale kuku 25 ulio anza nao jumla utakua na kuku 225. Baada ya miezi 6 kuku watakaotaga ni 170 kila mmoja akipata vifaranga 10 mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku (1700+20+55=1775) ukiuza kuku 1,000 kwa bei ya Tshs. 10,000 kwa kila kuku mmoja utapata Tshs. 10,000,000 (million kumi). Mwaka wa 2 majike 775 yakiangua vifaranga 10 kila mmoja utakuwa na kuku 7,550 mwisho wa mwaka ukiuza kuku 3,000 kwa bei ya Tshs. 10,000 utapata Tshs. 30,000,000 (million Thelathini) Hesabu hizi ni kwa makadirio ya chini sana kwani kwa kawaida kuku mmoja kama atatunzwa vizuri anaweza kuataga mayai kati ya 10 hadi 12 kwa mwezi.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment