Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayatarishi maisha yake.
Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote .
Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kam hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010.
Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu .

SOURCE:BBCSWAHILI
0 comments :
Post a Comment