Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.
Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya
kuteua wabunge wasiozidi 10.
Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.
Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
- Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
- Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
- Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
- Mhe. Janet Zebedayo Mbene
- Mhe. Saada Salum Mkuya
- Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
- Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
- Mhe. James Fransis Mbatia
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.
0 comments :
Post a Comment