Hatimaye kwa mara ya Kwanza Mtanzania
Mbwana Samatta atashiriki Ligi ya Ulaya kwa ngazi ya vilabu katika hatua
ya makundi akiwa na timu yake ya Genk ya nchini Ubelgiji na kuandika
historia kwa maisha yake na ya Tanzania
Mbwana Samatta
Samatta
ambaye amejiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita, ameifungia
timu hiyo magoli muhimu katika hatua zote za kufuzu hadi kufikia hatua
hiyo.
Katika mchezo wa leo ulioiwezesha kufuzu hatua hiyo ya makundi, Genk imeisambaratisha NK Lokomotiva Zagreb ya Croatia kwa mabao 2-0 na kuifanya ifuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kutoka sare ya 2-2 katika mchezo uliopita, uliopigwa nchini Croatia.
Mbwana Samatta alikuwa miongoni mwa wafungaji katika michezo yote miwili, ambapo katika mchezo wa leo, yeye ndiye aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 1 ya mchezo akimalizia kros ya Leon Bailey.
Bao la pili limefungwa na Leon Bailey dakika ya 50, na hadi mchezo unamalizika, Genk imebaki na mabao yake 2-0 na kufuzu hatua ya makundi ya ligi hiyo.
Droo ya makundi ya ligi hiyo ambayo pia itaihusisha timu ya Manchester United ya England itafanyika Ijumaa hii.
Licha ya kuifungia mabao muhimu katika ligi hiyo, Samatta pia ameanza kwa kasi katika ligi kuu nchini humo, ambapo hadi sasa yeye ndiye kinara wa ufungaji wa mabao, akiwa na mabao 4 kileleni.
Hatua hii ni nafasi nzuri kwa nyota huyo wa Tanzania ambaye ndiye nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kujitangaza yeye na nchi yake kwa mataifa mbalimbali ya Ulaya katika ulimwengu wa soka.
SOURCE:EAST AFRICA TV

0 comments :
Post a Comment