Kamishina
msaidizi wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdan amesema
bado wanamtafuta mmiliki wa kampuni ya Foreplan Juma Mwaka kama
walivyoagizwa na Naibu Waziri wa Afya.
Alisema vijana wake wapo kazini kuhakikisha wanampata ndani ya saa 24 kama walivyoagizwa hapo jana.
Hatua
hiyo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla la kumtafuta
baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika jengo hilo na kukuta huduma
zinaendelea.
CANZO:JICHO LA HABARY
0 comments :
Post a Comment