Kocha
Mkuu mpya wa Taifa Stars, Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart
Nooij anatarajiwa kuwasili nchini Jumamosi alfajiri (Aprili 26 mwaka
huu) tayari kwa ajili ya kuanza kazi ya kuinoa timu hiyo.
Nooij
(59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo
anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache
kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi
itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mart
Nooij ni raia wa Uholanzi, na ameshawahi kufanya kazi katika nchi ya
Mozambique kama kocha mkuu wa timu ya taifa, Burkina Faso U20, na pia
ameifundisha timu ya Santos ya Afrika ya Kusini.
About Omari Makoo
0 comments :
Post a Comment