-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 3) HII NI KAZI YA MIKONO YANGU


KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 3)
Jamaa mmoja ambaye alikuwa ni mfundi mjenzi,Aliajiriwa kwenye kampuni moja kubwa sana na kufanya kazi kwa muda mrefu sana huku akipata sifa mbali mbali kuhusu utendaji wake kuwa bora.Hakulewa sifa alizidisha utendaji wake na kufanya kampuni hiyo kupata tenda nyingi za ujenzi wa nyumba.
Alipofikisha umri wa kuingia uzee akaamua kuandika barua ya justaafu kwenye kampuni hiyo.
Mmiliki wa kampuni alimjibu kwamba wameridhia kustaafu kwake lakini walimuamuru amalizie ujenzi wa nyumba moja ya ghorfa ya mwisho katika ujenzi wake.Alichukizwa sana na tendo hilo la kuongezewa kazi nyingine wakati yeye alikuwa anataka astaafu.Hivyo aliamua kuifanya kazi hiyo kwa roho upande na kuifanya ovyo...sehemu ya mchanga mwingi anatia simenti nyingi na sehemu ya simenti nyingi anatia maji mengi sehemu ya chuma anaweka mbao na sehemu ya mbao imara anaweka za kawaida.....Aliffanya hivyo mpaka nyumba ikakamilika....alipomaliza alifurahi sana na kusema hapa sasa nimewakomoa vya kutosha.
Aliwasiliana na mabosi wake na kuwaambia kwamba kazi yao imeisha cha ajabu aliambiwa kwamba ofisi nzima itakuja kuangalia kazi hiyo kisha ataruhusiwa rasmi kustaafu...kwa kuwa alishaamua na liwalo na liwe akaamua kujikaza na kuwasubiri.
Baada ya masaa machache mabosi pamoja na wafanya kazi wengine wa kampuni walifika na kuanza kumpongoza kwa kustaafu kwakee kisha boss wake akamwambia hii ilikuwa ni surprise ya kampuni yao kwa utendaji wake bora ndani ya kampuni....Hivyo walikuja na hati za nyumba zikiwa na jina la jamaa pia wakamwambia funguo ulizonazo ni za kwako kutoka sasa hivyo wewe ni miliki halali wa nyumba hiii na hii ni zawadi yetu kwako.
JAMAA AKAANZA KULIA NA KUSEMA HII NI KAZI YA MIKONO YANGU
je kama ungelikuwa wewe ungefanayaje??????????
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment