-->

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA ZITTO KABWE BUNGENI LEO

Dondoo muhimu za nilichoongea Leo Bungeni
1. Hivi sasa Serikali ya 3 imejificha, ipo. Gharama ni zile zile. Sio lazima tuwe na Marais 3, hatujengi ikulu Mpya. Gharama za Wizara za Muungano zipo ndani ya Bajeti ya sasa ya Serikali mbili. Hakuna taasisi Mpya zaidi ya Tume za uwajibikaji nk.
2. Hatuhitaji kuongeza kodi, tunahitaji kuondoa ubadhirifu na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima. Tunapoteza Mapato lukuki kwenye misamaha ya kodi (theluthi ya mapato ya idara ya forodha inasamehewa, sawa na tshs 2 trilioni kwa mwaka), ukwepaji wa kodi (asilimia 5 ya Pato la Taifa inapotea, sawa na tshs 2.3 trilioni kwa mwaka ) na ubadhirifu mwingine uliokithiri. Hivyo udhibiti wa asilimia 50 tu wa misamaha ya kodi na ukwepaji kodi unaongeza mapato zaidi ya trilioni 2 ambazo Serikali ya Muungano inaweza kugawa kwa Washirika kwa miradi maalumu ya kitaifa.

3. Serikali 3 zitaweka Uwazi wa Mapato na zitaweka Uwajibikaji kwa serikali kutazamana zenyewe. Hizi za sasa zimejaa lawama sababu hakuna Uwazi. Naomba kuuliza, fedha za mapato kutoka TCRA lini zimeenda Zanzibar? Mawasiliano ni jambo la Muungano. Lini fedha za TCAA zimeenda Zanzibar? Gesi Asilia ni jambo la Muungano, hivi Zanzibar wanapata mgawo wa asilimia ngapi kutoka gesi ya Songosongo? Anga ni jambo la Muungano, fedha za chenji ya rada zimerudi, Zanzibar imepata kitabu hata kimoja? Mimi ni mwenyekiti wa PAC, najua haya ninayosema na hamtayamaliza katika S2 sababu ya confusion ya Muundo. Tatu ni Muundo unaoeleweka. Tukiamua zifanye kazi zitafanya.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment