Jamani kuweni makini na Accounts zenu za Facebook kwani siku hizi kumeibuka mtindo wa wezi wa mitandao ambao wana iba passwords za Facebook za watu na kisha kuzitumia katika utapeli kwa kuandika status ya kuwadanganya watu na kuwatapeli kwa kupitia account yako....
Nini wanafanya mpaka kupata password yako bila wewe kujua? Kuna njia nyingi wanazotumia kwa mfano hii ni njia moja ambayo hata mimi nimeshajaribiwa kama mara tatu lakini huwa nagundua mapema, Unaweza kuta kwenye inbox yako ya Facebook umetumiwa ujumbe kama huu hapa Chini:
"Habari yako , kuna watu fulani wanasambaza picha zako chafu , ingia hapa kuona hizo picha zako:...Link) "hapo wanakuwekea link ambayo ukiiclick inafungua page kama facebook hivi ila sio facebook na inakuomba Username na Password yako ya facebook sasa wewe kwa vile unataka kuona hizo picha unajikuta umeweka password yako na ukisha submit hakuna cha picha wala nini ila user name na password yako inakuwa imeshatumwa kwa hao wezi na hapo ndio wanaanza kazi ya kutapeli watu
0 comments :
Post a Comment