PICHA KUTOKA MAKTABA
KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 13)
Katika jiji la Dar es salaam katika miaka ya 2001 kijana mmoja ambae
alionekana kuwa na muonekano hafifu kutokana na kupigwa
kimaisha.Hakuchoka kutafuta kamwe,kila saa kumi na moja ya usiku tayari
alikuwa ndani ya magari yaendayo mashambani kwa ajili ya kwenda kuchukua
ndizi na kuja kuuza sokoni.
Kwa hakika alikuwa maarufu sana kwa ukarimu na huruma kwa watu pamoja na heshima kwa watu wenye rika zote.
Siku moja akiwa anaelekea kwenye stand ya daradara ziendazo mashambani
akaskia kerere za watu waliokuwa wakiita mwiziii mwiziii,akajaribu
kuangaza macho yake huku na huku kutizama wapi mwizi alipo pasina
kumuona....Alishangaa kuona umati mkubwa wa watu waliobeba mapanga,mawe
na silaha za jadi wakija upande wake.Kwa akili ya haraka haraka akajua
huenda mwizi amewapotea na wanakusudia kuja kumuuliza labda amekunjia
kona ipi......Ghafla mawe yakaanza kumlaki kijana yule huku wenye
mapanga wakimsogelea na kuanza kumshambulia vikali,Alijaribu kujitete
lakin haikuwa rahisi watu waliokuwa na hasira na wezi,Hawakumsikiliza
kabisa zaidi ya kumtwanga vitofa mpaka kupoteza fahamu,Damu nyingi
zilim-mwagika kisha raia wakaanza kuchanga pesa ya kununulia petroli ili
waweze kumchoma moto kabisa.Pesa ikatimia kisha akaagizwa kijana mmoja
aende akanunue petroli,kwa haraka sana alienda kisha na kurejea na dumu
lililojaa petroli alipofika kabla ya kumwagia kijana yule ndipo
alipowasili mmama mtu nzima kidogo ambae hakuwa na uwezo wa mbio
ingawaje yeye ndiye aliyeporwa simu pamoja na kipochi akiwa anaelekea
kazini.
Mmama huyo alishangaa kukuta kijana aliyelala chini si yule
aliyempora simu na kipochi ingawaje walifanana mavazi ya juu na chini.
Alilalama kwa kusema mmemua mtu siye Kwa Mungu na apa huyu siye
aliyeniibia ee Mungu wangu naomba unisamehe kwa hili....Alili kwa
uchungu mithili ya aliyefiwa na mumewe au mwanae lakini haikubadilisha
ukweli.....
Watu wote walianza kushangaa na kila mtu nafsi kumsuta
kwa kusababisha maumivu makali kwa mtu asiye na hatia...Wengi
walibubujikwa na machozi huku wasijue nini wafanye...kila mmoja akaanza
kuomba kivyake kwa Mungu ili ajaalie kijana yule asife.....
Wakati
kunaanza kupambazuka kijana alifungua macho na fahamu kurejea watu
wakaanza kufurahi na kuhisi Mungu amejibu dua zao ghafla kijana alianza
kukoroma na kukata roho.................
NA HUO NDIO ULIKUWA MWISHO WA KIJANA HUYO
FUNZO:SI KILA ANAEITIWA MWIZI BASI ANAHATIA,KAMWE HAUTOWEZA KUISHI KWA AMANI UKIGUNDUA KUWA UMEITOA ROHO ISIYO NA HATIA..
TUACHE SHERIA ZIFUATE MKONDO WAKE
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment