-->

VIGOGO WA TANESCO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUITIA HASARA YA MIL 200 SERIKALI

tanescologo_e4d1c.jpg
Aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Semtutu na wenzake wanne, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka mawili yakiwamo ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. milioni 200.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa Fedha, Lusekeo Kasanga, Mwanasheria Godson Ezekiel na Mkandarasi Martin Abraham.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isdore Kyando alidai kuwa washtakiwa walifanya makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.
Kyando alidai kuwa katika shitaka la kwanza, Desemba, mwaka 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo jijini Dar es Salaam washtakiwa walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha Mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment