Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia akiongea katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto).
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto) akiwa amekumbatia na Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia mara baada ya kumaliza uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bw. Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa, Bw. Nicola D’Elia wakionyesha alama ya 'POA' mara baada ya kumaliza uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Watu waliofika katika uzinduzi huo.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni
ya simu ya mkononi TIGO imetangaza kuingia katika ushirikiano na
kampuni ya mtandao wa kijamii Facebook ambapo wateja wake wote nchini
watapata huduma ya Facebook bure kwa lugha ya Kiingereza na kwa mara ya
kwanza, katika lugha ya Kiswahili kupitia simu zao za mkononi.
Hii ni
mara ya kwanza kwa Facebook kupatikana bila malipo kwa mtandao wowote
eneo la Afrika mashariki, kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego
Gutierrez.
Akizungumza
katika tafrija ya uzinduzi wa ushirikiano huo jijini Dar es Salaam,
Gutierrez alisema: “Ushirikiano huu unamaanisha kwamba wateja wa Tigo
kwa mara ya kwanza watakuwa na uwezo wakutumia Facebook kupitia simu zao
za mkononi bila kukatwa gharama yeyote katika utumiaji wa data, hivyo
kuwawezesha kuungana na watumiaji wapatao milioni 2 wa mtandao huo wa
kijamii waliopo nchini Tanzania kati ya watumiaji bilioni 1.2 duniani
kote.”
Gutierrez
aliongeza: “Hii ni kwa mara ya kwanza mtandao wowote mkubwa wa kijamii
umeweza kupatikanika kwa Kiswahili, lugha ya taifa inayotumika na
Watanzania na wingi wa watu walio katika kanda ya Mashariki, Kati na
Kusini mwa Afrika. ”
“Facebook
imekuwa chachu kubwa ya utumiaji wa data kwa mitando ya simu. Kwa
ushirikiano huu wa kipekee, Tigo imepewa kipaumbele kuliko mitandao
mingine katika kuwaletea wateja wengi ladha mpya ya utumiaji waintaneti
na mitandao ya kijamii kupitia lugha ya Kiswahili. Hii ndio maana halisi
ya maisha ya kidigitali, pia inatimiza malengo yetu ya kuwashawishi
wateja wengi zaidi wa Tigo kutumia data katika matumizi yao ya
mawasiliano ya kila siku.”
Mkakati huu wa ushirikiano ni muendelezo wa mpango wa Facebook unaoitwa Internet.org uliozinduliwa na muasisi wa kampuni hiyo, Mark Zuckerberg.
Gutierrez
alisema, “Huduma hii mpya itafungua milango mipya kwa Watanzania na
watumiaji wengine wa Kiswahili kupata fursa za kibiashara, kielimu, na
nyinginezo za kijamii na kiuchumi duniani kote.”
Ukiondoa
nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya,
Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi, Kiswahili pia kina zungumzwa katika
maeneo ya Malawi, Somalia, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na
Msumbiji.
Kwa
uzinduzi huu, Tanzania taifa linayojulikana kama chimbulo la lugha ya
Kiswahili, inayofahari ya kuwa nchi ya kwanza katika ukanda huu
kutangaza lugha hii kimataifa, mafanikio ambayo hatuna budi yanatokana
na ushirikiano kati yaTigo, kampuni mama ya Millicom na Facebook.
Hii ni
mara ya pili kwa kampuni ya Facebook na Millicom kushirikiana katika
kuzindua huduma ya Facebook kupitia simu bure ambapo Tigo nchini
Paraguay walizindua huduma hii kwa mara ya kwanza Desemba 2013 katika
lugha ya kiguarani inayotumika nchini humo.
Mkurugenzi
wa Facebook wa Ushirikiano na Ukuaji wa Kimataifa Nicola D’Elia
alisema, “Tunayo furaha kushirikiana na Tigo kwa mara nyingine tena kwa
kuwapatia Watanzania wengi zaidi uwezo wa kuwasiliana kupitia utumiaji
bure wa data katika app ya Facebook na tovuti ya simu, na sasa katika
lugha ya Kiswahili.”
0 comments :
Post a Comment