-->

JULIUS S.MTATIRO ATOA YAKE YA MOYONI KUHUSU CCM NA YANAYOENDELEA KWENYE MCHAKATO WA KATIBA

 
-§-Baada ya kutoa ulinzi mkali na kuhakikisha kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemaliza ziara yake ya kuzurura katika sehemu mbalimbali nchini kikifanya Mikutano ya hadhara ya kuwakashifu na kuwapinga na wajumbe wa Tume ya Katiba, Kuipinga Rasimu ya Katiba na Kuyapinga Maoni ya Wananchi Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya Hadhara haswa likionekana kuulenga zaidi ule wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) uliopangwa kufanyika leo jumamosi tarehe 19/04/2014 kule Zanzibar.

Inashangaza sana!

Mikutano ya harara ya CCM kuzurura katika sehemu mbalimbali nchini imefanyika pasipo wasiwasi wala hofu yoyote ya kiusalama, ila kusikia vyama na wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wanataka kufanya mkutano wao wa hadhara kule Zanzibar na baadae katika sehemu nyinginezo nchini Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya hadhara kwa kile inachokisema kwamba ni kwasababu za kiusalama katika hali inayoonekana ni njia mojawapo ya kuwabana na kuwakomoa UKAWA wanaopigania na kutetea maoni ya wananchi yaliyomo katika rasimu halali ya Katiba haswa muundo wa muungano wa Serikali3.

Taarifa hiyo imetolewa jana wakati jeshi hilo likijua wazi kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina chochote cha kupoteza kwasababu kimemaliza ratiba yake ya kuzurura katika sehemu mbalimbali nchini kikifanya Mikutano ya hadhara ya kupinga vikali Tume halali ya Katiba, Rasimu halali ya Katiba na maoni halali ya Wananchi yanayotaka muundo wa Muungano wa Serikali Tatu na kutaka muundo wa Muungano wa Serikali2 inayotokana na Tume hewa, Rasimu hewa iliyobeba Maoni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa matakwa na maslahi ya chama hicho.

Maswali Kuntu

1. Hivi hili ni Jeshi la Polisi au Jeshi la Polisi la kulinda matakwa na maslahi ya Chama Cha Mapinduzi ??!!

2. Kwa kudhibiti na kuzuia mikutano ya hadhara haswa ile ya wapinzani na wale wote ambao wako kinyume na matakwa ya Chama Cha Mapinduzi kwa kile jeshi hilo inachokuwa ikisingizia mara kwa mara kwamba ni sababu za kiusalama ilihali ikitoa uhuru kwa Chama Cha Mapinduzi kufanya mikutano yake kwa uhuru na pasipo vikwazo wala visingizio ni sababu ya msingi kutolewa na jeshi hilo??!!

3. Je, Jeshi la Polisi linatambua kwamba moja ya wajibu na jukumu lake kubwa ni kulinda usalama wa raia na mali zao wakati wote na hata pindi mikutano hiyo ya hadhara inapokuwa ikifanyika ??!!

4. Mbona inapokuja kwenye suala la:

(a) Kupambana na Majangili wanaoua Tembo na Vifaru wetu,
(b) Kupambana na Magaidi wanaolipua mabomu hovyo na kuua raia wasio na hatia,
(c) Kupambana na Vigogo na wale wote wanaojihusisha na Biashara haramu ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina zote jeshi hilo limekuwa dhofli hali yaani dhaifu kabisa ??!!

(Kupambana na raia wasio na hatia ufanisi 100%)

5. Kwanini mara zote sababu na visingizio vya jeshi hilo kuhofia usalama zitolewe tu katika mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani na si chama tawala (CCM) ??!!

6. Je, ikisemwa kwamba hata vurugu, majerui na mauaji ambayo yamekuwa yakitokea katika mikutano ya vyama mbalimbali vya Siasa haswa CHADEMA chanzo ni Jeshi hilo la Polisi tutakataa ??!!
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment