KISA CHENYE MAFUNZO
Kuna nchi mmoja ilikuwa ikitawaliwa kifalme lakini mtindo wake wa kumpata kiongozi ulikuwa ni wa kipekee kwani
Maflme alitakiwa kukubali kwamba ataongoza kwa muda wa miaka mitano kisha atapelekwa kwenye kisiwa chenye wanyama wakali kilchopo karibu na mji huo.
Maflme wa kwanza alikubali na kuongoza kwa mika mitano kisha alichukuliwa mkuku mkuku na kupelekwa kwenye kisiwa hicho chenye wanyama wakali,hivyo aliuawa na wanyama hao.
Kisha wakatangaza kutafuta Malme mwingine kurithi kiti hiko huku masharti yakiwekwa wazi kwamba baada ya miaka mitano utapelekwa kwenye kisiwa chenye wanyama wakali ambacho kinafahamika kwa kila mtu.
Mfalme alipatikana na kukubali kuongoza kwa miaka mitano na baada ya hapo kupelekwa kwenye kisiwa cha wanyama wakali.maflme huyo aliamua kufurahia maisha kwa kuoa wanawake wengi na kuagiza kila aina ya chakula pamoja na kila aina ya mavazi.Miaka mitano ilipofika alilia sana kwani alijua kifo chake kimewadia.Hakuna aliyemuonea huruma,alichukuliwa na kupelekwa kwenye kisiwa hicho na kuuliwa na wanyama hao.
Kisha wakarudi kwa wananchi na kuwatangazia kwamba anayetaka ufalme kiti kipo wazi ila akubali kwamaba baada ya miaka mitano atapelekwa kwenye kisiwa hicho.
Kijana Omari mwenye umri mdogo kabisa alinyoosha mkono na kusema yeye yuko tayari kuwa mfalme,walimuhurumia na kumwambia kwamba wewe bado mdogo huogopi kufa,Yule kijana alisisitiza kuutaka ufalme.Basi wakaaamua kumpa huku wakistaajabu kijana Omari kwa nini haogopi kufa.
Yule kijana Omari mwaka wake wa kwanza akaagiza pale mjini watengeneze ZOO(sehemu ya kufugia wanyama kwa ajili ya maonyesho)hivyo wanyama wakali wote walikusanywa kutoka kwenye kile kisiwa na kuletwa Mjini kwenye ZOO.
kisha mwaka uliofuata akaagiza kusafishwa kwa kisiwa na kuanza ujenzi wa nyumba za taifa kwenye kisiwa hiko.
Mwaka wa tatu wa utawala wake akaagiza kujengwa kwa daraja la kisasa kutoka pale mjini kwenda kwenye kisiwa.
Kisha mwaka wa nne akaboresha miundombinu katika kisiwa kwa kuweka bara bara safi na kuweka umeme na kusambaza maji na huduma mbali mbali za kijamii kwenye kisiwa.
Alipoikisha mwaka wa tano walikuja wale viongozi wengine na kumwambia umemaliza kipindi chako hivyo tunakupeleka kwenye kile kisiwa akasema haina shaka niko tayari kwenda.
FUNZO:UNACHOKIPATA LEO WEKEZA KWA AJILI YA KESHO
KUMBUKA KUNA MAISHA BAADA YA HAPA DUNIANI
JE UMEJIANDAAJE??????????????
0 comments :
Post a Comment