PROFESA LIPUMBA : TANZANIA INAWEZEKANA KUWA NA SERIKALI TATU
Tanzania inaweza kuwa na serikali tatu na kuzimudu iwapo itazingatia nidhamu ya matumizi ya fedha na kuachana na ubadhirifu, wizi na ufisadi kwenye fedha za umma.
Mwanazuoni maarufu, Profesa Ibrahimu Lipumba, ameliambia Bunge Maalum la Katiba na kusisitiza kuwa shida si fedha bali ‘ulaji’ uliokithiri ndani ya serikali.
Alikuwa akitoa ufafanuzi wa maoni ya wachache ya Kamati Namba 10, yanayounga mkono uwapo wa serikali ya shirikisho.
Alipingana na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kuzindua Bunge hilo pamoja na maoni ya wajumbe wengi kuwa serikali tatu ni kuongeza gharama na taifa haliwezi kuiendesha.
Prof. Lipumba alitaja sababu kubwa ya Serikali kukosa fedha za kujiendesha kuwa ni ubadhirifu na misamaha ya kodi isiyozingatia uhalisia.
Akipinga madai kuwa kuendesha serikali tatu itakuwa ni gharama kubwa na kusema: “Gharama kubwa tulizo nazo zinatokana na ubadhirifu, ufisadi na wizi wa fedha za umma.”
Alinukuu taarifa ya mapatio ya fedha za umma ya mwaka 2010/2013 inayoonyesha kuwa asilimia kati ya 35 na 45 ya matumizi ya serikali hayana tija, hivyo fedha zinapotea kiholela kila mwaka.
Aidha Profesa Lipumba alikosoa muundo wa utafutaji fedha za bajeti ya Serikali ya Muungano aliosema umekuwa tegemezi kwa wafadhili bila kuweka mikakati ya kujikwamua na utegemezi.“Theluthi moja ya matumizi ya serikali hiyo ikiwa daima ni mikopo na misaada kutoka nje kwa miaka yote,” alibainisha.
“Kimsingi serikali haitoi fedha za matumizi kugharamia maendeleo na inategemea wafadhili na mikopo. Lakini pia bajeti zinazotengenezwa na Bunge hazitekelezi,” alisema Profesa Lipumba.
Aliwaambia wajumbe kuwa bajeti inayotekelezwa ni tofauti na iliyopitishwa Dodoma.
“Nasema tena matatizo yetu si kwamba tuna serikali mbili au tatu bali tatizo kubwa ni ukosefu wa misingi mizuri ya kusimamia matumizi ya fedha za umma, ubadhirifu na kukosa nidhamu ya bajeti,“ alisema Profesa Lipumba

0 comments :
Post a Comment