Lusajo anakuwa mchezaji raia wa Tanzania, mwenye elimu zaidi ya
wachezaji wote wanaocheza Ligi Kuu kwa sasa ingawa anazidiwa kidogo na
kipa wa Toto Africa, Erick Ngwegwe ambayo iko Ligi Daraja la Kwanza.
STRAIKA wa Yanga, Reliants Lusajo ndiye mchezaji msomi kuliko wote ndani
ya kikosi hicho lakini amekiri kwamba ana changamoto kubwa ya kupata
namba ya kudumu. Lusajo amemaliza masomo yake ya Shahada (digrii) katika
Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kilichopo mkoani Kilimanjaro alikokuwa
akisoma Shahada ya Ugavi (Bachelor of Arts in Procurement). Mchezaji
huyo amekosa michezo 10 ya ligi msimu huu kwa kuwa alikuwa akimalizia
ripoti yake ya Utafiti (Research) kama sehemu ya masomo yake na mwezi
ujao atatunukiwa shahada yake ya kwanza kwenye mahafali ya chuo hicho.
Lusajo anakuwa mchezaji raia wa Tanzania, mwenye elimu zaidi ya
wachezaji wote wanaocheza Ligi Kuu kwa sasa ingawa anazidiwa kidogo na
kipa wa Toto Africa, Erick Ngwegwe ambayo iko Ligi Daraja la Kwanza.
Uchunguzi wa Mwanaspoti umebaini kwamba wachezaji wengi wa klabu za Ligi
Kuu wameishia darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na
wachache wana elimu ya cheti. “Nlifurahi kucheza kwa mara ya kwanza Ligi
Kuu baina ya Yanga na Mgambo JKT, ligi ni ngumu na inahitaji mtu
kufanya kazi kwa juhudi kubwa. “Yanga ina wachezaji wazuri na wenye
uzoefu mzuri, nafikiri kwa kwa sasa nimemaliza masomo yangu hivyo
nitahakikisha nafanya kazi yangu ya mpira kwa kujituma,” alisema Lusajo.
CHANZO:~MWANASPOTI-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment