Rubani
msaidizi wa ndege iliyopotea namba MH370 alipiga simu yake ya mkononi
wakati ndege ikiruka chini chini kupita pwani ya magharibi mwa Malaysia.
Wachunguzi
wamegundua kwamba simu hiyo ilipigwa kutoka kwenye simu ya mkononi ya
Fariq Abdul Hamid wakati Boeing 777 ikiruka chini chini karibu na kisiwa
cha Penang, kaskazini mwa pwani ya magharibi ya Malaysia.
Gazeti la
The New Straits Times limeripoti leo kwamba ilifahamika ndege hiyo,
ilikiwa na watu 239 ndani yake, ilikuwa ikiruka chini chini kiasi cha
minara ya mawasiliano iliyokuwa karibu kuweza kunasa ishara za Fariq.
Simu hiyo ilikatika ghafla,
hata hivyo imefahamika kwamba mawasiliano yalirushwa na kituo kidogo cha
mawasiliano kilichopo kwenye jimbo la Penang.
Gazeti hilo lilisemwa kwamba
haikuweza kujulikana mara moja Fariq alikuwa akimpigia nani 'kutokana na
chanzo cha habari kutotaka kuweka bayana taarifa zaidi za uchunguzi.'
Liliongeza: "Mnara wa kampuni ya mawasiliano ulinasa simu hiyo aliyokuwa akijaribu kupiga.
"Kuhusu kwanini simu hiyo
ilikatika, inawezekana sababu ndege hiyo ilikuwa ikienda kwa kasi mbali
na mnara huo na haikuweza kupata mawasiliano kwenye mnara unaofuatia,"
gazeti hilo lilisema, likinukuu vyanzo vya habari.
Gazeti hilo liliongeza kwamba
imebainika pia kwamba mawasiliano ya mwisho ya Fariq yalikuwa kupitia
WhatsApp na kwamba yalifanyika majira ya Saa 5:30 usiku wa Machi 7, muda
mfupi kabla hajapanda ndege hiyo kuanza safari ya masaa sita kwenda
Beijing, China.
The New Straits Times lilisema
lilielezwa kwamba ukaguzi wa kumbukumbu kwenye simu ya Fariq ulionesha
kwamba mtu wa mwisho kabisa kuongea naye ilikuwa 'mtu wake wa kawaida
(namba iliyokuwa ikijirudia rudia katika orodha ya simu zake
alizopiga).'
Simu hiyo ya mwisho, lilisema
gazeti hilo, ilipigwa sio zaidi ya masaa mawili kabla ya ndege hiyo
kuruka saa 6:41 usiku wa Machi8 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kuala Lumpur.
Vyanzo tofauti vililieleza
gazeti hilo kwamba ukaguzi kwenye simu ya Fariq ulionesha kwamba
mahusiano na simu hiyo aliyopiga simu hiyo ya mwisho kabla ya kupanda
ndege hiyo yalikuwa 'adilifu'.
"Hii ni matokeo ya kawaida kwa simu hiyo kuwa imezimwa.
"Wakati fulani, hatahivyo,
wakati ndege hiyo ikiwa angani, kati ya Igari na eneo hilo karibu na
Penang (muda mfupi kabla ya ndege hiyo kupotea kwenye rada), laini hiyo
'iliunganishwa tena'."
Gazeti hilo lilisema kwamba
uunganishwaji haumaanishi kwamba lazima simu hiyo kwamba ilipigwa.
Inawezekana pia ni matokeo ya simu hiyo kuwa imewashwa tena.
Jana ilionekana kama kisanduku cheusi kinaweza kuwa kimepatikana chini katika Bahari ya Hindi.
Kituo cha redio cha 6PR
kilituma ujumbe katika twitter ugunduzi huo, kikimnukuu mtaalamu wa anga
Geoffrey Thomas, ambaye alibainisha kinasa taarifa hicho cha ndege hiyo
hatimaye kimepatikana zaidi ya mwezi mmoja baada ya Boeing 777 kupotea.
Waziri Mkuu wa Australia Tony
Abbott, ambaye yuko nchini China, alisema watafutaji wana 'uhakika'
ishara hizo zilizopatikana zilikuwa kutoka kwenye kisanduku cheusi
kutoka kwenye ndege ya MH370.
"Hakika sitaki kusema taarifa zaidi ya hapo kwa wakati huu... kama ishara ya heshima kwa watu wa China na familia zao."
0 comments :
Post a Comment