IKIWA ni rahisi au vigumu kujigundua
kama unauwezo wa kupata ujauzito au la, au kwa mwanaume kama ana uwezo
wa kumpa mwanamke mimba au la.
Tatizo la kutofanikiwa kupata ujauzito kwa mwanamke linahusiana moja kwa moja na kuwepo na tatizo kwa mwanaume.
Unaweza kusema kama una tatizo hili endapo unaishi katika mahusiano ya
kutafuta ujauzito kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mafanikio.
Ili mwanamke apate mimba ni lazima awe na sifa za kupata ujauzito, na
ili mwanaume aweze kumpa mwanamke mimba ni lazima awe na sifa za kumpa
mwanamke mimba.
Matatizo haya yapo kwa pande zote mbili.
Wakati wa kutafuta ujauzito, ni vema mwanamke na mwanaume washirikiane
kwani mwanaume unaweza kujiona huna tatizo kumbe ukija kupima mbengu
zako utajikuta unatatizo kubwa.
Matatizo kwa mwanamke
Mwanamke mwenye tatizo la kutopata ujauzito anaweza kuwa na mojawapo ya matatizo haya yafuatayo;
Atakuwa amekaa na mume au yupo katika mahusiano ya kutafuta mtoto kwa
zaidi ya mwaka lakini hakuna mafanikio, hulalamika maumivu ya chini ya
tumbo mara kwa mara au yanaweza yasiwepo, maumivu ya hedhi, kuvurugika
mzunguko na kutoona ute wa uzazi.
Wengine hawana hamu
ya tendo la ndoa au kutojihisi raha wakati wa tendo, maumivu wakati wa
tendo au kutokwa na uchafu ukeni wakati mwingine huambatana na muwasho
na harufu.
Anakuwa na historia aidha ya kutumia njia za
uzazi wa mpango, kuharibu au kutoa mimba, historia ya kuzaa, au
kufanyiwa upasuaji wa aidha uzazi au mirija. Ingawa wengine hawana
historia hizi.
Nini cha kufanya?
Endapo
utahisi una matatizo ya kutopata ujauzito na unazodalili kama hizo hapo
juu au huna, basi ni vizuri umuone daktari wa magonjwa ya matatizo ya
uzazi katika hospitali za mikoa. Uchunguzi utafanyika kuangalia mfumo
wako wa homoni au vichocheo vya uzazi, vipimo vya kizazi na mirija na
vingine ambavyo daktari atashauri.
Uchunguzi na matibabu huchukua muda mrefu, ni vema kufuatilia kwa makini.
Athari kubwa zinazotokea mara nyingi katika uzazi kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya mayai.
Mvurugiko wa mfumo wa homoni, matatizo ndani ya kizazi ambayo yanaweza kuwa uvimbe au maambukizi.
Uwezekano wa kutibiwa na kufanikiwa upo endapo utazingatia.
Matatizo ya uzazi kwa mwanaume
Mwanaume kama atazingatia uchunguzi na tiba naye anaweza kufanikiwa
ingawa akigundulika kama anatatizo tiba yake huchukua muda mrefu.
Uchunguzi wa mwanaume ni kuangalia mbegu za uzazi na kupima korodani.
Mwanaume unaweza kujifahamu kama unatatizo endapo utakuwa na dalili
zifuatazo; siyo lazima zote lakini mojawapo, upungufu wa nguvu za kiume,
kuishi na mwanamke zaidi ya mwaka mmoja lakini hakuna mimba,
kutoa manii nyepesi sana na zenye harufu mbaya, manii nyepesi hutoka
mara moja ukeni unapomaliza tu tendo la ndoa.
Maumivu
ya muda mrefu ya korodani, maumivu ya kiuno, maambukizi ya mkojo ya mara
kwa mara, uvutaji wa sigara kwa muda mrefu, unywaji wa pombe kali, na
matumizi ya madawa ya kulevya mfano bangi na mirungi na mengineyo.
Nini cha kufanya?
Matatizo haya hutibika kwa daktari wa matatizo ya uzazi kwenye
hospitali za mikoa. Vipimo vya mbegu za uzazi vitafanyika kuangalia
kiwango cha mbegu na ubora wake kama zina uwezo wa kutungisha mimba.
Vipimo vingine itategemea na uwepo wa matatizo mengine ya uzazi kwa
mwanaume kama kuwahi kumaliza tendo la ndoa, kushindwa kufanya tendo la
ndoa, upungufu wa nguvu za kiume, uchovu mkali baada ya tendo la ndoa,
maumivu ya kiuno, korodani na maumivu ya njia ya mkojo. Wahi hospitali
kwa uchunguzi na tiba.http://bekamtanzania.blogspot.com
Home
/
afya
/
makala
/
usiyoyajua
/
DONDOO ZA AFYA:DALILI ZA MWANMKE AMBAYE HAWEZI BEBA UJAUZITO NA NJIA ZA KUJITIBU
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment