Sevilla
imefanikiwa kuichapa Benfica kwa penalti na kushinda taji la Europa
League katika mchezo wa fainali uliopigwa jana kwenye dimba la Turin,
likiwa ni taji la tatu kwa mashindano hayo ndani ya misimu tisa.
Benfica,
wamepoteza katika fainali saba za mashindano ya Ulaya walikuwa
wanalisaka taji la kwanza tangu mwaka 1962 lakini juhudi za Wareno hao
zingalizaa matunda lakini shambulizi la wisho la Lima halikuwa na tija kwao.
Kevin
Gameiro angaliweza kuifungia klabu yake baada ya mlinda mlango wa
Sevilla Beto kuokoa mikwaju ya Oscar Cardozo na Rodrigo huku Carlos
Bacca, Stephane Mbia, ambaye yupo kwa mkopo akitokea Queens Park
Rangers, na Jorge Moreno wangaliifungia Sevilla lakini hawakuwa makini.
Mbrazil
Lima na Luisao wangaliweza kuipatia Benfica bao lakini mlinda mlango
mzaliwa wa Lisbon Beto alifanya juhudi za juu kuhakikisha timu ya mji
aliozaliwa haipati kitu kwa kuzuwia mikwaju ya Cardozo na Rodrigo.
Sevilla iliwachapa wenzao wa Uhispania Espanyol kwa matuta na kutwaa taji hilo mwaka 2007, ikiwa ni miezi 12 baada ya kuichapa Middlesbrough na kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza, ambapo awali mashindano hayo yalijulikana kama Uefa Cup.
0 comments :
Post a Comment