Maelezo –Zanzibar 20/5 2014
SERIKALI
ya Mapinduzi Zanzibar imetakiwa kutoa elimu kwa wananchi ili kujua
umuhimu wa utalii nchini na kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatoa huduma
iliyobora na kuimarisha uchumi wa Taifa.
Akiwasilisha
Ripoti ya Kamati ya Wenyeviti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu
Hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2014/2015 Mwenyekiti wa
Wenyeviti Hamza Hassan Juma amesema ni muhimu kwa Serikali kuimarisha
ulinzi kwenye maeneo yote ya utalii na kuondosha vitendo vya uahalifu
ili kuhakikisha kuwa sekta hiyo inaimarika.Amesema
ipo haja Serikali kuimarisha miundombinu itakayowawezesha watalii
kupata huduma bora wanapoingia nchini ikiwemo kuimarisha viwanja vya
ndege, bara bara, kuongeza vivutio vya utalii na maeneo ya kutembezea
watalii, kuweka miji katika hali ya usafi pamoja na kuimarisha ulinzi.“Kwa
kuwa nchi yetu inategemea zaidi mapato yake kutokana na utalii, bado
hatujaekeza ipasavyo katika kutoa taaluma ya kutosha kwa ngazi zote,
Chuo chetu cha Utalii hakijaweza kutoa Shahada kwa wahitimu jambo
linalosababisha nafasi za juu katika ngazi ya ajira kuchukuliwa na
wageni na vijana wetu kubakia katika ngazi za chini”, alieleza Mhe.
Hamza.
Aidha
Kamati hiyo imeitaka Serikali kudhibiti ujenzi uanaoendelea maeneo ya
Mjimkongwe kwani umeanza kupoteza uasilia wa majengo yake kwa kujengwa
majengo ya kisasa jambo ambalo linaweza kuiondoa Zanzibar kwenye miji
yenye Urithi wa Kimataifa.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo ameomba Serikali kuandaa mpango wa matumizi bora
ya ardhi ili kuyalinda maeneo yote ya kilimo pamoja na kuyaongezea wigo
wa ruzuku na pembejeo kwa mazao ili kuwahamasisha wakulima kuongeza
kilimo na kupunguza nakisi ya uagizaji chakula kutoka nje.
“Pamoja
na Serikali kueleza kuwa uchumi wetu unatarajia kuimarika katika mwaka
ujao kwa kuimarisha mazingira mazuri ya biashara lakini suala hili
inabidi kutekelezwa kwa vitendo na sio kwa maneno ya kwenye vitabu tu
kwa kupunguza urasimu kwa wawekezaji hasa wazalendo kwa kuwaondolea
vikwazo wanapoamua kuwekeza”, alifahamisha.
Akizungumzia
mpango wa maendeleo wa Bajeti, Mh. Hamza ameitaka Serikali kuimarisha
huduma za Hospitali za Mjini na Vijijini ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya
Mnazimmoja ambayo ndio kimbilio la wananchi wengi wa Zanzibar
Ameeleza
kuwa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, pamoja na kuwa na madaktari bingwa
wa fani tofauti, imekuwa ikipokea wagonjwa wachache wanaotumia Bima ya
Afya ukilinganisha na Hospitali za binafsi.
Amesisitiza
kuwa Kamati yake imeitaka Benki ya Watu wa Zaznibar (PBZ) kuanzishe
huduma ya kadi ya VISA na Master ili kuwa na wigo mpana wa kutoa huduma
zake.
“Benki
ya Watu wa Zanzibar wakianzisha huduma hii itaweza kuwavutia wateja
wengi hasa wale wakumbwa ambao wengi wao ni wafanya Biashara, ”alisema
Hamza.
Hamza
Hassan amesema kwa upande wa mapato imebainika kuwa Taasisi
zinazokusanya mapato huwasilisha fedha zote katika mfuko mkuu wa hazina
jambo ambalo hupelekea Taasisi hizo kushindwa kutekeleza vyema majukumu
yao kutokana na uhaba wa fedha wanazopatiwa
Kutokana
na hali hiyo, amesema kamati yake inazishauri Serikali kuzipatia
Taasisi hizo aslimia ya makusanyo yake ili ziweze kutekeleza
changamoto zinazowakabili.
“Tunaomba
Taasisi kama hizo, aidha zipangiwe utaratibu wa kupatiwa asili mia
fulani yaani Retaintion ili ziweze kujimarisha na kujenga uwezo wa
kukusanya zaidi ili kuongeza mapato ya Serikali”,alisema Hamza Hassan.
Ameisisitiza
kwa Serikali kufuatilia kwa karibu ukusanyaji wa mapato ya Taasisi
inazozipa ruzuku kwa lengo la kujipunguzia mzigo kwa zile Taasisi ambazo
zina uwezo wa kujitegemea.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
0 comments :
Post a Comment