-->

ARJEN ROBBEN,MULLER NA HUMMEL KUTUA MAN UNITED

Robben na Muller kuelekea Old Trafford,Kalou kurudi Uingereza.Meneja mtarajiwa wa klabu ya Manchester United,Louis van Gaal ameonyesha kuwahitaji nyota wawili wa Bayern Munich,Thomas Muller na Arjen Robben pamoja na beki wa Borussia Dortmund,Mats Hummels wakiwa ndiyo mipango yake ya awali.
Mholanzi huyo atatangazwa rasmi wiki ijayo kuchukua mikoba ya David Moyes aliyeachishwa kazi katika klabu hiyo ya Old Trafford kufuatia kutofanya vizuri katika kipindi chake cha miezi 10 klabuni hapo.
Van Gaal ameonekana kutoa mapendekezo yake kwa mashetani wekundu hao kuhusu suala zima la usajili wakati akiwa inaindaa timu ya Taifa ya Uholanzi inayotaraji kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Liverpool na Arsenal zimeingia kwenye vita ya kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Lile,Salomon Kalou ambaye aliwahi kuchezea klabu ya Chelsea ya Uingereza.

Washika bunduki walionyesha kuvutiwa na raia huyo wa Ivory Coast tangu katika dirisha dogo la mwezi Januari lakini hawakufanikiwa kupata saini yake.
Bayern Munich wameonekana kuvutiwa na David Luiz na wamepanga kuwapa Chelsea ofa ya mshambuliaji Mario Mandzukic kama sehemu ya kubadilishana.

Beki huyo raia wa Brazil anahusishwa na kutaka kujiunga na Barcelona mara baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika hivyo mabingwa hao wa Ujerumani watakuwa wameingia kwenye vita kali dhidi ya klabu hiyo ya Camp Nuo ambayo imekuwa ikihaha kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Meneja wa Liverpool,Brendan Rodgers anatazamia kupata saini ya kinda wa Hamburg,Jonathan Tah mwenye miaka 18 ambaye anacheza beki wa kati pamoja na beki wa kushoto wa Sevilla,Alberto Moreno mwenye umri wa miaka 21 ambaye alichukua kombe la Europa League huku akiwa anatakiwa pia na Chelsea.

Manchester United wamepeleka ofa kwa kiungo wa Roma,Kevin Strootman.Mashetani wekundu hao wanamatumaini ya kumnasa raia huyo wa Uholanzi kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 25.
Meneja wa Everton,Roberto Martinez anatazamia kumchukua winga wa Tottenham,Andros Townsend ili ajiunge na klabu hiyo ya Merseyside huku akiwa anajiandaa kupata upinzani kutoka kwa meneja wa Newcastle,Alan Pardew.

Spurs wanaweza kujiandaa kufanya biashara ya kumuachia raia huyo wa Uingerezaa ambaye hajaitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia Brazil.
Liverpool pia wanamtupia macho kiungo mchezeshaji wa Valencia,Daniel Parejo.Wekundu hao wa Anfield wana malengo la kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Majogoo hao wa Anfield watataka kuzishinda Everton na Arsenal katika kupata saini ya nyota huyo mwenye miaka 25 ambaye anatakiwa kulipiwa pauni milioni 20 ili kuweza kuvunja mkataba wake na klabu hiyo ya Uhispania.

Chelsea imeungana na Liverpool pamoja na Arsenal katika vita ya kuwania saini ya kinda wa MK Dons,Dele Alli ambaye ana umri wa miaka 18 na amekuwa akisemwa kuwa ndiye Steven Gerrard.
Manchester City watazishinda Chelsea na Manchester United kwenye vita ya kumuwania beki wa Roma,Mehdi Benatia.

Raia huyo wa Morocco ambaye anamudu vilivyo beki ya kati anapatikana kwa kiasi cha Euro milioni 19.5 ambazo ni sawa na pauni milioni 16.

Meneja wa Liverpool,Brendan Rodgers ataimarisha kikosi chake majira ya joto huku kukiwa na nyota kadhaa chipukizi wakitaraji kuondoka Anfield.
Suso amekuwa kwa mkopo katika klabu ya Almeria anahusishwa kutaka kuuzwa pamoja na Luis Alberto na Iago Aspas wote wataondoka pia klabuni hapo.
Ctedit.Kandanda.co.tz
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment