Mtoto mmoja ambae baba ake alikuwa ni mtu mwenye pesa kiasi,mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka 6,Siku moja baba alikuja na gari na kupaki nje ya nyumba yao.Ghafla mwanae akatoka nje pasina yeye kuwa na fikra kwamba anakwenda kufanaya nini nje,Yule mtoto alisogelea gari kisha kuwanza kulichuna gari kwa kutumia koa.
Baba alipokuwa ndani alipata wazo la kuja kumtizama mwanae nje na ndipo alipokuta amelichuna gari hilo kwa kutumia koa.Baba alichukia sana alimpiga yule mtoto mpaka kumvunja vidole vya mkono wa kulia na mtoto kuzimia.Alipoona hivyo alimuaisha hospitali huku mama wa mtoto akilia pasina kunyamaza.
Walipokutana na daktari,wakaambiwa mtoto wonu amevunjika vibaya hivyo hawezi kuungika hivyo tunapaswa kuvikata hivi vidole ili kuweza kumsaidia mtoto wenu.Baba hakuwa na budi ilibidi akubali mwanae kukatwa vidole vilivyovunjika....
Mtoto wao akazinduka na kukuta vidole vyake vya mkono wa kulia vimekatika.Hivyo akamuuliza baba yake.
Mtoto:Baba vidole vyangu vitakuwa tena?
Baba:mwanangu..............(akapatwa na kigugumizi na kushindwa kuongea)
Baba mtu akaamua kuondoka hospitalini hapo hukua akiwa analia kwa alichokifanya.Alipofika nyumbani akaenda kutizama alichokuwa akichora mwanae na kukuta maandishi yanayo someka
DAD I LOVE YOU
Baba akaanguka chini na kuzimia pale pale
FUNZO:kabla haujaamua jambo hebu fikiri mara mbili kwani kuna vitu havina spea
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment