Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini kuwapo
kwa wanafunzi wanaopatiwa mikopo katika vyuo vitano nchini licha ya
kufeli au kuahirisha masomo yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa
mwaka wa fedha 2012/13, mikopo ya kiasi cha Sh. milioni 201.5 ilitolewa
kwa wanafunzi hao.
Taarifa hiyo imevitaja baadhi ya vyuo na kiasi cha fedha kila kimoja
kwenye mabano kuwa ni Vyuo Vikuu katika nchi za Algeria, Cuba ( milioni
132), Urusi (milioni 9.6), Chuo Kikuu cha Dodoma (milioni 43.9) na Chuo
Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) (milioni 28.9).
Pia, imebaini wanafunzi kupewa mikopo bila kuzingatia matokeo ya
mitihani yao kama ilivyoainishwa katika kanuni za fedha za Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu nchini ( (HESLB), hivyo kukosekana kwa fursa kwa
wanafunzi waliostahili kupata mikopo.
Imeeleza kuwa hali hiyo imesababisha matumizi mabaya ya fedha kwenye
vyuo na hasara kwa umma kutokana na Bodi kushindwa kukusanya fedha
kutoka kwa walionufaika na mikopo hiyo.
SOURCE:MATUKIO NA VIJANA
SOURCE:MATUKIO NA VIJANA
0 comments :
Post a Comment