Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
CHUO
cha mafunzo ya taaluma ya Jeshi la polisi Moshi (MPA), kimewafukuzisha
mafunzo jumla ya wanafunzi wa uaskari 212, kutokana na sababu za
kughushi vyeti vya elimu ya sekondari..
Hayo
yamesemwa leo na Mkuu wa Taaluma na Utumishi wa jeshi la Polisi,
Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye katika kikao na waandishi wa
habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha mafunzo ya taluma ya
Polisi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Kamishna
Andengenye alisema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Baraza la
Mitihani la Taifa (NECTA), lilifanya uhakiki wa Vyeti vya wanafunzi wote
3,415 waliojiunga na mafunzo hayo Desemba mwaka jana ambapo waligundua
kuwa wanafunzi 212 kati yao hawakuwa na sifa kutokana na
"Katika
kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwa na askari wenye ueledi na uaminifu
kwa raia na taifa kwa ujumla, tuliendelea na zoezi la kuhakiki vyeti kwa
kushirikiana na baraza la mitihani la taifa, ambapo
vyeti vya wanafunzi wa uaskari 212 kati ya walioripoti vimeonekana kuwa ni vya kughushi," alisema Andengenye.
Alisema
kufuatia hali hiyo pamoja na kuwaachisha mafunzo wanafunzi hao 212,
Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na taasisi nyingine linaendelea
kufanya upelelezi ili kuhakikisha kuwa hatua za kisheria zinachukuliwa
dhidi ya wanafunzi hao na maaskari wote watakaobanika kughushi vyeti.
0 comments :
Post a Comment