KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 24)
Nchini Ugiriki katika miaka ya (469 - 399 BC), Socrates mmmoja miongoni mwa wanafalsafa wakubwa duniani alifuatwa na moja miongoni mwa watu wake wa karibu akija wangu wangu mithili ya mtu mwenye jambo jipya mdomoni mwake.
Kisha akasema "Socrate unajua nini nimeskia kuhusu mwanafunzi wako"(akiwa na shauku ya kutaka kumletea umbea Socrate)
Alishangazwa sana na majibu ya Socrate
Socrate:Kabla haujaniambia nataka nikupea jaribio moja linaitwa The Triple Filter Test.
The filter test?akauliza kwa mshangao
Ndio tena kichujio cha kwanza ni
1.Je unachotaka kuniambia ni cha kweli?na una uhakika kwamba unachotaka kuniambia ni cha kweli
Hapana sina uhakika nimeskia tu(yule kijana akasema)
Ok kwa hiyo haufahamu kwamba ni cha kweli au laa!
Haya twende kichujio cha pili
2.Kuhusu uzuri,je unachotaka kuniambia ni kuhusu jambo jema au mambo mazuri ya mwanafunzi wangu?
Hapana si kuhusu jambo zuri(akajibu yule kijana)
Socrate:Ok kwa hiyo ni jambo baya bila shaka na bado unashahuku ya kuja kuniambia
Kijana akaanza kuhisi kwamba amedhalilika
Kisha Socrate akaendelea kumuuliza yule kijana,basi ngoja tujaribu na hiki kichujio cha tatu
3.Kuhusu faida ya jambo unalotaka kuniambia,Je unachotaka kuniambia mimi kuhusu mwanafunzi wangu lina faida kwangu?
Hapana halina faida kwako
Kisha Socrate akamalizia:sasa kama jambo unalotaka kuniambia halina ukweli,sio jambo zuri na wala halina faida kwangu kwa nini unataka kuniambia
Kijana aliishiwa nguvu na kuhisi fedheha
FUNZO:Akija mtu anataka kukwambia jambo hebu mpime na vipimo hivi kwanza
je kuna funzo lingine nawe umeliona kutoka kwenye kisa hiki,weka hapo chini
0 comments :
Post a Comment