-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 21)

Mmama mmoja wa kijiji fulani alisikia jambo fulani la aibu kuhusu jirani yake kutoka kwa rafiki yake,Yule mama baada ya kupata taarifa hiyo akaanza kuisambaza na hatimae ikasambaa kila sehemu na kupelekea chuki na uhasama mkubwa kati ya yeye na yule jirani yake.
Baada ya muda kupita akaja kupata taarifa za uhakika kuhusu jambo lile,Kumbe jirani yake hausiki kabisa,Akaona ni vyema atafute njia ya kuweka sawa katika jamii ili sasa waelewe tofauti na vile alivyosambaza awali.Alifikiria mbinu tofauti lakini hakupata jibu kabisa na ndipo alipoamua kwenda kuomba ushauri kwa bibi mmoja ambae husifika sana kwa hekima na busara.
Alipofika kwa yule bibi,akaamua kumwambia ukweli yule bibi na kwamba nilisambaza jambo baya lilofanywa na jirani yangu baada ya kuambiwa na mtu niliyemuamini sasa nimegundua kwamba hakufanya kabisa wala hakuna kitu kama hiko,Hivyo akamuomba ushauri kwamba afanye nini ili aweke mambo sawa.
Yule bibi akamjibu kwamba nenda sokoni nunua kuku kisha mpe mtu akuchinjie kisha mpunyue manyoya yote kisha unaporudi nyumbani nenda unamwaga manyoya hayo mpka nyumbani kwako.Kwa kuwa alikuwa na shida akaamua kufanya kama alivyoelekezwa na yule bibi kisha akarejea kwa bibi.Yule bibi akamwambia lala leo kisha kesho amka uyakusanye yale manyoya uliyoyatupa barabarani kutokea sokoni.Kesho kulipokucha alifanya kama alivyoagizwa cha ajabu hakubahatika kupata manyoya yote isipokuwa matatu tu.
Kisha yule bibi basi mjukuu na ujifunze kwa mfano huu kwamba yale manyoya yamepeperuka na mengine yamefagiwa hivyo huna uwezo wa kuyarejesha,vivyo ilo jambo baya uliliomsambazia jirani yako huwezi lisafisha kwani sasalinawasambazaji wengi kuliko ulivyodhani.
FUNZO;Si kila unaloliskia unapaswa kusema
              Hata kama ni kweli ,Jaribu kuficha aibu ya mwenzako
WEKA NA MENGINE HAPO CHINI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment