Sababu zilizowafanya Kambi Rasmi ya Upinzani, kutoka nje ya Bunge jana jioni wakiongozwa na Kiongozi wake, Freeman Mbowe, zimewekwa hadharani kuwa ni madai ya wenzao wa CCM walishajipanga kupitisha Bajeti hiyo, huku pia wakilalamikia ratiba ya mkutano huo wa 15 wa Bunge.
Hata hivyo, Spika Makinda alisema ratiba ya mkutano huo ilipangwa na Kamati ya Uongozi ambayo pia
inamshirikisha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, kwa hiyo iliridhiwa na kamati hiyo.
Akijibu hoja ya IPTL, Waziri Muhongo alisema upo ushahidi kwamba wapinzani wamepewa fedha.
“Picha za CCTV zimeonesha wakisaini huko huko IPTL. Kwa kuwa hawapo, tusubiri tutaona ukweli,”
alisema Muhongo jana wakati akijibu hoja za wabunge na kusema hakupenda kulizungumzia suala hilo kwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alishasema tusubiri uchunguzi wa Takukuru na CAG.
Alisema suala hilo si jambo jepesi, na kwamba hata yeye anazo hati mbalimbali zinazofikia gari lenye uzito wa tani moja na kushangazwa na wanaotamba kuwa wana hati mbalimbali za mgogoro huo.
“Watu wamekuja hapa wanakurupuka tu, sio watu makini, hivi vitu vya mahakama. Unajidhalilisha, hawa ni mamluki wa kifedha,”alisema Profesa Muhongo.
Alisema tayari kati ya waliowasilisha hati zao kwa Spika, mojawapo ni feki, na kuonya kuwa Bunge lisitumike kama mahakama. Alisema ni lazima suala la IPTL lifike mwisho kwa sababu linadhalilisha nchi na linakwamisha uwekezaji.
“Watu msikurupuke na vitu msivyovifahamu, ni aibu sana. Itabidi wakati mwingine watu tuone vyeti vya watu hapa,”
alisema Prof. Muhongo.
Aliwataka wote ambao wanapinga uamuzi uliotolewa na Mahakama, kwenda mahakamani kupinga badala ya suala hilo bungeni na kuudanganya umma wakati wanadai kuna kuheshimu mihimili ya Dola. --- wavuti.com imenukuu habari hii kutoka gazeti la HabariLeo
0 comments :
Post a Comment