-->

KISA CHENYE MAFUNZO(VOL 22)

Mzee mmoja alikuwa anadaiwa  na mtu mkubwa sana kwenye kijiji fulani,kiwango cha pesa alichokuwa anadaiwa kilikuwa kikubwa sana kiasi kwamba hakuweza kabisa kuilipa pesa hiyo na hata akipewa miaka miwili bado asingweza kuilipa kutokana na ukubwa wa deni hilo pamoja na hali yake ya maisha,
Hivyo siku moja yule jamaa mkubwa kwenye serikali ya kijiji akaamua kuita wanakijiji na viongozi wengine wa kijiji na kumpa masharti yule mzee mbele ya wanakijiji wote.
Ardhi ya kijiji hicho ilkuwa imejaa kokoto nyingi sana,hivyo alipoona watu wote wamefika akaanza kutoa mashrti kwa mdeni wake kwa kumwambia kwamba atatoa mabegi mawili ya kuwekea pesa lakini mabegi hayo ataweka mawe  mawili,jiwe moja likiwa jeupe na lingine jeusi kisha akasema binti yako

1.akichagua jiwe jeusi basi ataolewa na mimi na deni lote ntakusamehe
2.Akichagua jiwe jeupe hataolewa na mimi na debi lote litakuwa limesamehewa
3.Akigoma kuchagua wewe baba yake utafungwa jela.
Baada ya masharti hayo yule kigogo akaokota mawe mawili chini kwa haraka sana na kuyaweka kwenye mabegi mawili kwa haraka,Kwa jicho kali na la haraka yule binti akiwa mbali alifanikiwa kuona mawe mawili aliyoyaokota yule kwamba yote ni mawe meusi tupu.Kisha akaitwa na kuambiwa achague begi moja kati ya yale mawili.Yule mdada akiwa amejaa woga na kuona ule ujanja alioutumia yule mzee wa kuweka mawe meusi tupu ili afanikiwe kumuoa kirahisi akavuta pumzi na kusogelea yale mabegi..................
Kisha akachukua begi na kutoa jiwe moja kwa haraka na kujifanya limemponyoka na kuchanganyika na mawe mengine pale chini.Watu wakiwa kwenye tahamaki yule binti akasema kwa kuwa alisema kunajiwe jeusi na jeupe na mimi nilillochagua limeanguka basi tutizame begi la pili tujue nilichagua lipi?Basi wakafungua begi la pili na kukuta jiwe jeusi hivyo ikaonekana kwamba amechagua jiwe jiupe hivyo baba yake ikaamuliwa kusamehewa deni na mtoto wake kutoolewa na yule mzee.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment