Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SAA
chache zilizopita, shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza kuwa
ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16
badala ya 14 za sasa.
Afisa
habari wa TFF, Boniface Wambura katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari mchana huu ameseme mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana
(Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo ya
kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuongeza ushindani
katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi nyingi zaidi za
mashindano. Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi ya msimu wa
2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi 182.
Baada
ya taarifa hiyo, mtandao huu umekuwa ukipokea simu na ujumbe mfupi wa
simu kuuliza namna jinsi timu hizo mbili zitavyopatikana.
Ili
kujibu swali hilo, mtandao huu kwa kujali wasomaji wake umelazimika
kumtafuta kwa mara nyingine Afisa habari wa TFF kupata majibu ya swali
hilo.
Wambura
ameuambia mtandao huu dakika chache zilizopita kuwa cha kwanza kamati
ya utendaji umeridhia kuongezeka kwa timu, lakini kinachofuata ni
marekebisho ya kanuni.
“Cha
kwanza, timu zimeongezwa katika msimu wa 2015/2016 kutoka 14 kwenda 14,
lakini cha pili kinachofuata ni kwamba kanuni zitafanyiwa marekebisho”.
“Kamati
imeridhia mapendekezo ya kuongezwa timu, kwahiyo mapendekezo hayo
inabidi yaende rasmi kwa ajili ya marekebisho ya kanuni”.
“Marekebisho hayo yataonesha timu zinapandaje na zinashuka vipi”. Amesema Wambura.
Kwa
maelezo hayo ya Wambura, wadau wafahamu kuwa mapendekezo yamepitishwa,
lakini mpaka sasa haijulikani namna ya kuzipata timu zilizoongezwa mpaka
marekebisho ya kanuni yatakapofanyika.
Kwasasa sheria inasema timu tatu kutoka ligi daraja la kwanza zitapanda ligi kuu na timu tatu kutoka ligi kuu zitashuka daraja.
Kuhusu
idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia
uamuzi mapendekezo katika eneo hilo baada ya kwanza kupata maoni ya
klabu za VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu
zitakutana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Mapendekezo
ya Kamati ya Mashindano ni kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee
kuwa watano kama ilivyo katika kanuni za sasa za VPL.
0 comments :
Post a Comment