-->

WAMILIK WA FACEBOOK KUTAKA KUINUNUA WHATSAPP

facebook a6957
Facebook na WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana.
Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa. Chanzo: bbcswahili
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment