-->

KITU KINACHOZANIWA KUWA NI BOMU CHALIPUKA MKUNAZINI,ZANZIBAR

 Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu kinachozwaniwa ni mripuko katika eneo la Mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majadhara na hakuna uharibifu wa majengo katika eneo hilo.   
 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mhe. Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini, Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la tukio na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo wakati wa mripuko huo.  

Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la mripoko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.

Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu.
PICHA NA ZANZINEWS 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment